Monday, February 29, 2016

SAMSUNG GALAXY S7; KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA PAMOJA NA PICHA!

Siku chache zilizopita Samsung walitambulisha toleo jipya Samsung Galaxy S7 pamoja na Samsung Galaxy S7 Edge. Simu hizi mbili zinatofautia kigodo sana. Tofauti kubwa iliyopo kati ya hizi simu ni design lakini mambo mengine mengi yanafanana.

Leo tutaongelea Samsung Galaxy S7. Tutazungumzia umbo lake, uwezo wake wa kuhifadhi vitu, ukubwa wa display, android gani inatumia pamoja na uwezo wa camera.



Kitu cha kwanza kabisa ambacho Samsung Galaxy S7 kinayo ni uwezo wa kutoingia maji. Hii ina maanisha utaweza kutumia simu yako hata sehemu yenye mvua au hata ukiwa sehemu za starehe kama beach au kwenye swimming pool.



Samsung Galaxy S7 pia ina sehemu ya kuweka memory card. Baada ya watumiaji wa samsung Galaxy S6 kulalamika sana kwa kutokuwa na sehemu ya kuweka memory card, Samsung wameamua kuwafurahisha wapenzi wa simu zake kwa kuweka sehemu ya kuweka memory card hadi yenye ukubwa wa 200GB.



Samsung Galaxy S7 inakuja moja kwa moja kutoka kwenye box na android (6.0.2)marshmallow. Hili ni jambo zuri kwa wale wapenzi wa samsung kwakuwa wataweza kupata mambo mazuri kama Now On Tap pamoja na muonekano mzuri na speed kubwa pale wanapotumia S7 kwenye shughuli zao za kila siku.

Samsung Galaxy S7 ina kioo chenye ukubwa wa 5.1-inch screen na 2,560x1,440-pixel resolution pamoja na processor ya Qualcomm Snapdragon 820 pamoja na 4GB ya RAM. Samsung Galaxy S7 pamoja na Samsung Galaxy S7 Edge zote zina camera ya nyuma yenye 12 megapixel.

Samsung Galaxy S7 inakuja na fast charging pamoja wireless charging. Kwa wale wenye S6 basi watakuwa tayari wanajua raha ya fast charging na wireless charging.



Jambo lingine ambalo limetokea kuwavutia watu wengi ni Always-on. Always on ina maanisha simu yako ikiwa haitumiki basi display itakuwa inakuonyesha tarehe, mdaa huku ikiwa inatumia kiasi kidogo sana cha charge. Pia Samsung wanawawezesha watumiaji wa S7 na S7 Edge kuweza kulipa kwa kutumia mfumo wa Samsung Pay.



Endelea kutazama picha tofauti za Samsung Galaxy S7







Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment