Monday, February 22, 2016

JINSI YA KUFANYA SCREENSHOT ZA KIJANJA KWENYE SIMU YAKO YA ANDROID

Screenshot imekuwa ni njia nzuri sana ya ku share na marafiki zako jambo flani. Wengi wetu tumekuwa tukifanya screenshot kila siku kwenye simu zetu za android na kuwatumia marafiki au kwa ajili ya kumbukumbu lakini hatuzifanyi kijanja.

Leo tutaongelea app moja ambayo itakusaidia kuzifanya screenshot kwenye simu yako ziwe za kijana na zenye mvuto zaidi. Kwa mfano tazama picha mbili chini na utagundua picha moja ni screenshot ya kawaida na picha nyingine ni screenshot ambayo ina uhalisia zaidi na yenye mvuto.





Una weza jiuliza picha ya pili nimeifanyaje mpaka imekuwa na muonekano huo?. Jibu ni kwamba natumia app inayoitwa Screener. Unaweza download hii app kwa kutumia link chini kisha install kwenye simu yako
https://play.google.com/store/apps/details?id=de.toastcode.screener

JINSI YA KUTUMIA SCREENER KWENYE SIMU YAKO YA ANDORID

STEP 0

Baada ya kuiweka screener kwenye simu yako, ifungue na kisha bonyeza menu iliyopo juu upande wa kushoto na utapata muonekano kama picha chini

STEP 1

Bonyeza kipengele kinachosema flat kisha chagua aina ya simu unayo tumia. Mfano mimi natumia S5 kwa hiyo nimechagua Samsung Galaxy S5 kama picha inavyo onekana chini

STEP 2

Bonyeza alama ya jumlisha kisha nenda kachague picha au screenshot amabyo ungependa itokee kwenye frame ya simu uliyochagua kwenye Step 1. Baada ya hapo bonyeza kialama cha mshale kilichopo juu kulia kisha utapata muonekano kama picha chini. Bonyeza save kama unataka kuiweka kwenye simu yako au bonyeza share kama unataka kuwatumia marafiki.



Mpaka hapo utakuwa unaweza kuzifanya screenshot zako kuwa na mvuto pamoja na uhalisia zaidi. Kama unapenda kazi zetu unaweza ukatufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment