Sunday, July 20, 2014
(MAELEKEZO) JINSI KUONGEZA EMOJI NA KUPATA EMOJI TOFAUTI KWENYE WHATSAPP
Emoji ni vipicha vidogo ambavyo huwa vinapatikana sana kwenye zile apps za kuchat kama Whatsapp, viber, tango na nyingine nyingi. Kama wewe unapenda kupata emoji tofauti zaidi ya zile zilizopo kwenye whatsapp nitakupa maelekezo jinsi ya kufanya ili kuongeza emoji kwenye simu yako.
Haya maelekezo ni kwa watu wanaotumia simu za android kwanzia version 4.0. Endapo una android chini ya hapo basi unatakiwa ku-update simu yako au kuweka custom rom ambayo itakuwezesha kupata android 4.0.
Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha jinsi emoji zako zitakavyokuwa kwenye simu yako
VIGEZO VYA KUZINGATIA KABLA YA KUONGEZA EMOJI KWENYE SIMU YAKO
1) Simu yako inatikiwa iwe na exposed Framework. Kama huna exposed installer na ungependa kuiweka kwenye simu yako basi tembelea HAPA ili kujua jinsi ya kuweka exposed framework kwenye simu yako. Kama hujui exposed framework inaonekana vipi kwenye simu yako basi tazama picha chini
Note: simu lazima iwe rooted ili kuweza kuweka exposed framework kwenye simu yako. Kama hajui jinsi ya ku-root simu yako toa comment chini na utapewa maelekezo zaidi.
2) Hakikisha kwenye simu yako umekubali kipengele kinachosema "allow installation from unknown source". Kama bado ujafanya hivyo basi nenda kwenye settings halafu security kisha tick kibox kinachosema "allow installation from unknown source".
JINSI YA KUONGEZA EMOJI KWENYE SIMU YAKO YA ANDROID
1) Download module HAPA kisha install kwenye simu yako.
2) Fungua exposed framework installer kwenye simu yako kisha nenda kwenye kipengele cha modules halafu chagua Whatsapp emoji replacer
3) Restart simu kisha nenda kwenye list ya application zako kisha fungua whatsapp Emoji Kisha choose emoji style
4) Baada ya kuchagua emoji style chagua apply theme on the go kisha sema ok.
Done. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka emoji nyingine kwenye simu yako.
Toa comment kama una swali. Piga +255716203029 au +255753618318 kama ungependa usaidiwe. Gharama zitatozwa (Tsh 25,000 tu.)
Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment