Thursday, July 24, 2014
(MAELEKEZO) JINSI YA KUWEKA DYNAMIC NOTIFICATION KWENYE SIMU YA ANDROID
Dynamic Notification ni njia inayokuasaidia kupata notification wakati simu yako ikiwa iko locked. Hii inamaanisha unaweza kusoma messages, kuona missed calls au emails wakati simu yako ikiwa locked.
Kuweka Dynamic Notification ni rahisi sana endapo utakuwa umeweka exposed framework kwenye simu yako. Kabla sijatoa malekezo jinsi ya kuweka Dynamic Notification ni vizuri kukupa vigezo vya kuzingatia kabla ujaweka
VIGEZO VYA KUZINGATIA KABLA YA KUWEKA DYNAMIC NOTIFICATION KWENYE SIMU YAKO
1) Simu yako inatikiwa iwe na exposed Framework. Kama huna exposed installer na ungependa kuiweka kwenye simu yako basi tembelea HAPA ili kujua jinsi ya kuweka exposed framework kwenye simu yako. Kama hujui exposed framework inaonekana vipi kwenye simu yako basi tazama picha chini
Note: simu lazima iwe rooted ili kuweza kuweka exposed framework kwenye simu yako. Kama hajui jinsi ya ku-root simu yako toa comment chini na utapewa maelekezo zaidi.
2) Hakikisha kwenye simu yako umekubali kipengele kinachosema "allow installation from unknown source". Kama bado ujafanya hivyo basi nenda kwenye settings halafu security kisha tick kibox kinachosema "allow installation from unknown source".
JINSI YA KUWEKA DYNAMIC NOTIFICATION KWENYE SIMU YAKO YA ANDROID
1) Nenda kwenye playstore kwenye simu yako kisha search DYNAMIC NOTIFICATION halafu install kwenye simu yako.
2) Nenda kwenye settings kisha nenda kwenye accessability kisha enable dynamic notification
3) Fungua exposed framework installer kwenye simu yako kisha nenda kwenye kipengele cha modules halafu chagua
Tazama baadhi ya picha zikionyesha simu yangu ikiwa na dynamic notification
Done. Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka dynamic notification kwenye simu yako.
Toa comment kama una swali. Piga +255716203029 au +255753618318 kama ungependa usaidiwe. Gharama zitatozwa (Tsh 25,000 tu.)
Kama umependa kazi yetu usiache kutulike kwenye facebook yetu na follow us kwenye google+
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment