Thursday, February 26, 2015

JINSI YA KUBADILI SAMSUNG GALAXY S3 IWE KAMA NOTE 4


Kwa wenzangu wale ambao wanatumia Samsung galaxy s3 GT I9300 wanaweza update simu zao na kuweka mfumo wa Samsung Galaxy Note 4.

Kwa sasa Samsung Galaxy S3 inatumia android 4.3. Endapo uta update na kutumia Rom ya note 4 basi simu yako itatumia android 4.4.4



Wengi watakuwa wanajiuliza Samsung Galaxy S3 itawezaje kuwa kama Note 4? Jibu ni rahisi sana. Kupitia custom rom utaweza update s3 na kuwa kama note 4. Maelekezo niliyoyatoa chini yatakuwezesha kuifanya S3 na kuwa kama note 4.

Tazama video kwanza kuona jinsi samsung galaxy s3 ikiwa kama note 4


VIGEZO NA MASHARTI.


  1. HAKIKISHA SAMSUNG GALAXY S3 INATUMIA ANDROID 4.3 NA KUENDELEA
  2. MIMI SITAHUSIKA ENDAPO UTAARIBU SIMU YAKO
  3. UELEWA WA COMPUTER NI MUHIMU
JINSI YA SAMSUNG GALAXY S3 NA KUWA KAMA NOTE 4

STEP 0
Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy S3 GT I9300

STEP 1
Hakikisha una custom recovery kwenye simu yako. Kama una custom recovery tembelea link chini kujua jinsi ya kuweka custom recovery kwenye simu yako
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/06/maelekezo-weka-custom-recovery-kwenye.html

STEP 2
Download Dnote 4 rom kwa kupitia link chini kisha liweke hilo file ambalo ume downloads kwenye memory card ya simu yako
https://mega.co.nz/#!bN8QyRiC!t_-36RwX_PbJITrdD0-vX39F_14Git74uIeX0vnnkdM

STEP 3
Zima simu yako na kisha iwashe kwenye recovery mode. Ili kuwasha simu yako kwenye recovery mode unatakiwa ushikilie cha kuwashia, cha kupunguza sauti na Home button kwa pamoja hadi logo ya samsung itakapoonekana ndio uviachie.

STEP 4
Backup simu yako kwa kwenda kwenye kipengele cha backup and restore. Hakikisha unachagua kipengele kinachosema "backup to sdcard1"

STEP 5
Baada ya kumaliza ku backup, nenda kwenye kipengele cha kwanza kinachosema "install zip" kisha chagua kipengele kinachosema "install zip from sdcard1" kisha chagua lile file ambalo ulidownload kwenye step 2 (Bulldog74ts DN4 Port 2014 fix.zip)

STEP 6
Baada ya kumaliza kuflash Dnote 4 rom simu yako itajizima na kujiwasha. Kama haitajizima chomoa battery na kisha rudishia halafu washa simu yako.

Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka Dnote 4 rom kwenye Samsung Galaxy S3 na kuifanya iwe kama note 4.

Endapo utashindwa kuweka Dnote 4 rom kwenye Samsung Galaxy s3 unaweza kusaidiwa kwa kupiga namba +255716203029 na gharama ya Tsh 25000 itatozwa.

Tazama picha chini zikionyesha Muonekano wa Samsung Galaxy S3 ikiwa kama Note 4









No comments:

Post a Comment