LG G4 na Samsung Galaxy S6 ni top smartphones ambazo zimetoka mwaka huu. Simu hizi mbili zina chuana vikali kila kona kuanzia kwenye screen, sound, camera, software etc. Leo tutachambua mambo manne ambayo ni Display, Software, Design na Camera
Display
Kwenye upande wa Display, Samsung Galaxy S6 ina beba kioo chenye ukubwa wa 5.1-inch Super AMOLED kikiwa na resolution ya 2560×1440 pamoja na 577ppi wakati LG G4 ina beba kioo chenye ukubwa wa 5.5 inch kikiwa na resolution ya 2560×1440 na 538ppi (pixels per density). Hapa tunaweza kuona LG G4 ina kioo kikubwa kushinda Samsung Galaxy S6 lakini kioo cha samsung ndio bora na pia unaweza kutumia S6 bila matatizo hata ukiwa nje kwenye mwanga wa jua.Design na Hardware
Kwa upande wa Design na Hardware, Lg G4 inatumia chip ya Qualcomm Snapdragon 808 ambayo ni 64bit ARM wakati Samsung S6 ikitumia Exynos 7 Octa 7420 64bit ARM. Simu zote mbili zina RAM yenye ukubwa wa 3GB na uwezo wa LG G4 wa kubeba vitu ni 32GB wakati Samsung S6 ni 128GB.LG G4 inakupa uwezo wa kutumia memory card wakati Samsung S6 haikuruhusu kuweka memory card. Battery ya LG G4 ina ukubwa wa kiasi cha 3000 mAh wakati Samsung S6 ina ukubwa wa kiasi cha 2600 mAh. Battery ya S6 haitoki wakati ya LG G4 inatoka huku ikiwa na uwezo wa kutumika kwa mdaa mrefu kushinda ya Samsung S6
No comments:
Post a Comment