Monday, June 8, 2015

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA UJAWEKA CUSTOM ROM KWENYE SIMU YAKO


Custom Rom sio neno geni kwa wale wanaotumia simu za android. Baada ya android kuanzishwa na kufanywa open source kumechangia sana kuleta mambo makubwa kwenye simu za android kama vile custom rom.

Kwa kifupi custom rom ni kinyume cha stock rom. Stock rom ni ile ambayo unaikuta kwenye simu yako pale unapoinunua dukani. Endapo utaamua kuitoa stock rom kwenye simu yako na kuweka rom nyingine basi hapo utakuwa umeweka custom rom.



Kabla ujaweka custom rom kwenye simu yoyote inayotumia android yapo mambo machache unatakiwa uyajue. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia kabla ujaweka custom rom.


Warranty

Wengi tunajua kwamba unaponunua simu dukani unapewa warranty. Hii ina maanisha kwamba utaweza kurudisha simu yako endapo itakuwa na matatizo na kutengenezewa bure au kupewa simu nyingine. Endapo utaweka custom rom kwenye simu yako basi utakuwa umepoteza warranty yako na hutaweza kutengenezewa au kupewa simu nyingine endapo simu yako ikianza kukusumbua.

Root

Kabla ujaweka custom rom kwenye simu yako unatakiwa ujue kama simu yako ipo rooted au haipo rooted. Ili kuweza kuweka custom rom inakubidi u-root simu yako. Faida ya ku-root simu ni kwamba ina muezesha mtumiaji wa simu kupata ruksa ya kufanya chochote kwenye simu yake. Makampuni ya simu hupenda kumzuia mtumiaji wa simu asije akafanya mambo ya kipumbavu na kusababisha kuaribu simu yake. Tembelea link chini kujua kama simu yako ipo rooted au bado.
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/11/jinsi-ya-kujua-kama-simu-yako-imekuwa.html

Custom Recovery

Recovery ni kama application ambayo huwa inawekwa kwenye simu yako ili kukusaidia kuweka updates mpya za mfumo wa simu yako. Recovery ambayo inakuja na simu ikiwa mpya inaitwa stock recovery. Moja ya tatizo kubwa la stock recovery haimpi ruksa mtumiaji kuflash custom rom. Ili kuweza kuflash custom rom kwenye simu yako inakubidi kwanza utoe stock recovery kwenye simu yako na uweke custom recovery

Bootloader

Simu nyingi huwa zinakuwa na locked bootloader na yingine huwa zinakuwa na unlocked bootloader. Simu zenye locked bootloader huwa zinamzuia mtumiaji asije akachezea mafile muhimu ya simu yake kama boot image ambayo ndio muhimu sana kwenye utendaji kazi wa simu yake. Kwa mfano, simu kama HTC na Huawei huwa zina locked bootloader ili mtumiaji asije akaanza kuchezea mafile muhimu kwenye simu yake. Ili uweze kuweka custom rom inakubidi kwanza huakikishe kwamba bootloader yako ipo un-locked. Kama ipo locked itakubidi ku unlock bootloader kwanza.

Hayo ndio mambo muhimu ya kuzingatia kabla ujaweka custom rom. Kama unataka kuwekewa custom recovery kwenye simu yako au unataka ku-root simu yako na haujui ufanyaje unaweza wasiliana nasi kwa kupiga namba +255716203029 na gharama zitatozwa kiasi cha Tsh 25000 tu

Kwa wale wanaopenda blog yetu na wanataka tuendele zaidi basi usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment