Wengi wanaotumia simu ambazo zinauwezo mdogo na memory kidogo hujikuta wakishindwa kuweka apps nyingi kwenye simu zao na kusababisha kufuta baadhi ya vitu ambavyo hawaitaji ili waweze tu kuweka apps.
Wengi hukumbana na hii message "There is insufficient space on device " pale wanapotaka kuweka app kwenye simu za android kupitia playstore. Tatizo hili hutokea pale unapotaka kuweka app kwenye simu yako wakati internal storage ya simu yako imebaki kidogo sana na hatisholezi kuhifadhi file ambalo unataka kuweka
Zipo njia nyingi za kuweza kutatua hili tatizo. Njia ya kwanza ni kuhamisha apps ambazo zipo kwenye internal memory na kuzipeleka kwenye SD Card (memory card). Endapo unataka kuamisha file kwenda kwenye memory card, unatakiwa uende kwenye Setting kisha apps (application manager) kisha bonyeza app unayotaka kuiamisha na utaona muonekano kama picha inavyoonekana chini
Bonyeza sehemu iliyoandikwa Move to SD card. Kwa kufanya hivyo ina maanisha kwamba utakuwa umeamisha file kutoka kwenye internal memory ya simu yako na kulipeleka kwenye memory card ya simu yako.
Tatizo linakuja kwamba kuna baadhi ya apps ambazo huchukua nafasi kubwa sana kwenye simu yako na hauwezi kuziamisha na kuzipeleka kwenye SD card. Kwa mfano, Facebook, Chrome na Whatsapp ni baadhi ya apps ambazo hauwezi kuzipeleka kwenye SD card.
Kwa mfano chrome, unaweza kugundua kwamba imechukua kiasi cha 98.09MB kwenye internal memory ya simu yangu na kibaya zaidi siwezi kuiamisha chrome kwenda kwenye SD card. Kutoka na hili tatizo inatupelekea kuzungumzia njia ya pili ambayo ndio njia kuu itakayo kusaidia kuamisha app yoyote na kuipeleka kwenye SD card.
Hii njia ina hitaji uwe ume root simu yako. Kama bado uja root simu yako basi hautaweza kutumia hii njia. Kitu kingine kinacho itajika ni second partition kwenye SD card. Kama bado uja tengeneza second partition ya SD card yako unaweza kufanya hivyo kwa kutumia program kama Minitool, Paragon, Easeus etc. on Windows.
Note
Wakati unatengeneza second partition unatakiwa kutumia non-FAT file system (ext2, ext3, ext4 or f2fs)
Link2SD ni app ambayo inakuwezesha kuamisha app yoyote na kuipeleka kwenye SD card. Link2SD inapatikana kwenye playstore au unaweza ku download hii application kwa kutumia link chini
http://www56.zippyshare.com/v/zwVRrswp/file.html
Install Link2SD kwenye simu yako kisha ifungue. Grant super user access. Link2SD itafunguka na itakuonyesha app zote ambazo zipo kwenye simu yako. Chagua zile app ambayo unataka kuipeleka kwenye SD card. Kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa move to sdcard kama picha inavyo onekana chini
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuamisha app kutoka kwenye internal storage na kwenda kwenye SD card. Kwa kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kutatua tatizo la "THERE IS INSUFFICIENT SPACE ON DEVICE"
Kama unataka ku-root simu yako na haujui ufanyaje unaweza wasiliana nasi kwa kupiga namba +255716203029 na gharama zitatozwa kiasi cha Tsh 25000 tu
Kwa wale wanaopenda blog yetu na wanataka tuendele zaidi basi usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz
No comments:
Post a Comment