Smart Manager ni app ambayo ipo kwenye Samsung S6 na inakuwezesha kufanya mambo mbalimbali ili kuipa simu yako uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
Smart Manager ina vipengele vikuu vinne. Kipengele cha kwanza ni Battery,Ram,Storage na Ant virus. Picha chini inaonyesha vipengele vya smart manager
JINSI YA KUWEKA SMART MANAGER KWENYE SAMSUNG GALAXY S4
STEP 1
Hakikisha simu yako ipo rooted, pia install Es file Explorer kutoka kwenye playstore kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.estrongs.android.pop&hl=en
STEP 2
Fungua Es File Explorer kisha nenda kwenye settings, chini kabisa hakikisha kipengele kinachosema root explorer kinakuwa ON kama picha inavyo onekana chini
STEP 3
Donload SmartManager_S6_Albe95.zip kwa kupitia link chini kisha unzip (extract) hilo file na ndani yake utakuta folders mbili kama picha inavyo onekana chini
https://mega.co.nz/#!zsRywZzB!G7uzqsxviBQkUJ7_KbUhnMdDOgzoPtPb7l_10gf8wx4
STEP 4
Hamisha hayo ma folder mawili kisha yapeleke kwenye system/priv-app
STEP 5
Shikilia folder linaloitwa smart manager mpaka utakapopata muonekano kama picha chini
STEP 6
Nenda kwenye kipengele kinachosema more kisha utapata muonekano kama picha chini
STEP 7
Nenda kwenye kipengele cha properties kisha igilizia muonekano wa properties ambao unaonekana kwenye picha chini kisha bonyeza ok
STEP 8
Rudia ulichofanya kwenye step 5, step 6 na step 7 katika lile folder la pili ambalo linaitwa smartmanagersdk
STEP 9
Fungua ndani ya folder la smart manager kisha utakutana na folder linaloitwa lib na file linaloitwa smartmanager.apk. Rudia ulichofanya kwenye step 5, step 6 na step 7 katika lile folder la lib.
STEP 10
Shikilia file linaloitwa smartmanager.apk kisha nenda kwenye more kisha badilisha properties na zifanane na properties kama zinavyo onekana kwenye picha pichi kisha sema ok
STEP 11
Ndani ya folder la lib utakuta ma folder mawili (arm na arm 64) Kwa kila folder rudia kama ulivyofanya kwenye step 5, step 6 na step 7
STEP 12
Ndani ya folder la arm utakutana na mafile manne. Hakikisha unarudia step 5, step 6, na step 10 kwa kila file
STEP 13
Ndani ya folder la arm64 utakutana na mafile manne. Hakikisha unarudia step 5, step 6, na step 10 kwa kila file
STEP 14
Ndani ya folder la smartmanagersdk utakuta file linaloitwa smartmanagersdk.apk kisha rudia step 5, step 6, na step 10.
STEP 15
Baada ya kukamilisha yote hakikisha unazima simu yako kisha iwashe. Nenda kwenye list ya apps zako utaona smart manager app kisha ifungue na utapata muonekano kama picha chini
No comments:
Post a Comment