Wednesday, July 15, 2015

JINSI YA KUIFANYA SAMSUNG GALAXY S4 KUWA KAMA GALAXY S6


Samsung Galaxy S6 ni smartphone ambayo inasifika sana kwa sasa. Samsung Galaxy S6 inakuja na vitu vingi kama themes ambavyo hauwezi kuvikuta kwenye simu kama Galaxy S4. Leo tutaangalia jinsi ya kuifanya Galaxy S4 kuwa kama S6.

Hii ina maanisha kwamba simu yako ya S4 itakuwa na muonekano wa Galaxy S6 na utaweza kutumia app za Galaxy S6 kama themes, keyboard, browser, file manager, dialer, message app na vitu vingi ambavyo havipo kwenye Galaxy S4.



JINSI YA KUIFANYA SAMSUNG GALAXY S4 KUWA KAMA GALAXY S6


Vigezo na Masharti vya kuzingatia

  • 1: MIMI SITAHUSIKA ENDAPO WEWE UTAARIBU SIMU YAKO
  • 2: SOMA MAELEKEZO KWA UMAKIMI KABLA UJAJARIBI KWENYE SIMU YAKO
  • 3: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy S4 GT-I9505
  • 4: Hakikisha simu yako ina charge ya kutosha kuanzia 60%
  • 5: Simu yako iwe inatumia android 5 na kuendelea

STEP 0

Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy S4 GT-I9505 na sio vinginevyo. Pia hakikisha simu yako inatumia android 5(lollipop) kabla ujaendelea.


STEP 1

Hakikisha kwenye simu yako tayari umeweka custom recovery. Kama bado tembelea link chini kujua jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S4. Kama tayari umeweka custom recovery unaweza ukaendele kwenye step 2
http://phonetricktz.blogspot.com/2015/07/jinsi-ya-kuweka-custom-recovery-kwenye.html

STEP 2

Download ALBE95 LOLLIROM kwa kutumia link chini kisha baada ya kumaliza ku-download liweke hilo file kwenye memory card ya simu yako
https://mega.co.nz/#!O5xBCD5R!ViRlSpJTDybZI86K7ilb7KQsX-9afS5bmn4pHeqoeU0

STEP 3

Zima simu yako kisha iwashe kulekea kwenye recovery mode. Kama ujui jinsi ya kuwasha simu yako kulekea kwenye recovery mode tazama picha kisha soma malekezo chini ya picha


Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode bonyeza kitufe cha katikati (Home) + cha kuongeza sauti (Volume up) + na cha kuwashia (power) kisha vishikilie kwa pamoja mpaka utakapoana logo ya samsung kwenye screen yako kisha viachie vitufe vyote kwa pamoja.

STEP 4

Nenda kwenye kipengele kinachosema backup. Hakikisha una backup simu yako kabla ujaendelea.

STEP 5

Baada ya kumaliza backup, nenda kwenye kipengele kinachosema factory reset kisha fanya factory reset. Kisha nenda kwenye kipengele kinachosema wipe cache kisha wipe cache. Baada ya hapo nenda kwenye kipengele kinachosema advanced halafu chagua kipengele kinachosema wipe dalvik cache

STEP 6

Nenda kwenye kipengele kinachosema install zip kisha chagua kipengele kinachosema choose zip from sdcard1 kisha tafuta lile file ambalo uli download kwenye step 2 ambalo linaitwa Albe95_LolliROM_V4_0.zip. kisha install hilo file. Subiri mpaka simu yako imalize ku-install kisha washa simu yako. Simu itachukua kama dakika 11 ili kuwaka.

STEP 7

Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuifanya Samsung Galaxy S4 GT-I9505 kuwa kama Samsung Galaxy S6.

 Tazama picha chini zikionyesha Samsung Galaxy S4 GT-I9505 ikiwa na muonekano wa Samsung Galaxy S6

Home screen ikiwa kama ya s6

File manager ikiwa na muonekano wa s6

Keyboard ya S6

Ultra power saving mode kutoka kwenye S6

Mult-window kutoka kwenye S6

Themes Support kutoka kwenye S6


Endapo umeshindwa kufwatilia malekezo juu, na ungependa Samsung Galaxy S4 GT-I9505 iwe na muonekano wa Samsung Galaxy S6 unaweza wasiliana nasi kupitia namba +255684917346 na gharama zitatozwa kiasi cha Tsh 25,000 tu.

Pia unaweza kutufwata kwenye instagram kwa kutumia jina la phonetricktz

No comments:

Post a Comment