Thursday, July 9, 2015

JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S4 (GT-I9505)

Kwa wale wanaopenda ku-flash simu zao na kuzipa muonekano mzuri basi watakuwa wameshasikia kuhusiana na custom recovery. Custom Recovery ni njia ambayo inakuwezesha kutumia custom rom kwenye simu za android

Leo tutaongelea jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy S4 (GT-I9505). Jina la custom recovery ambayo tutaweka kwenye S4 (GT-I9505) ni TWRP recovery(Team Win Recovery Project)


Kujua aina ya recovery ambayo imekuja na samsung galaxy S4 unatakiwa kuizima simu yako kisha Bonyeza na kuvishikilia vyote kwa pamoja cha kuongeza sauti(Volume up) + cha katikati (Home) + Cha kuwashia (power) mpaka utakapoona logo ya Samsung kwenye screen kisha viachie na utaona recovery ambayo huwa inakuja na simu yako. Sasa sisi tunachofanya ni kuitoa hiyo iliyokuja na simu na kuweka TWRP recovery(Team Win Recovery Project)

Kabla sijatoa malekezo jinsi ya kuweka Team Win Recovery kwenye S4 (GT-I9505) ni vyema kukupa vigezo vya kuzingatia kabla ujajaribu kuweka custom recovery kwenye.

Vigezo na Masharti vya kuzingatia

  • 1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
  • 2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer
  • 3: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy S4 GT-I9505
  • 4: Unatakiwa uwe na computer inayotumia window

JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY S4 (GT-I9505)

STEP 0

Download Samsung drivers kwa kutumia link chini kisha install kwenye computer yako
http://developer.samsung.com/technical-doc/view.do?v=T000000117#none

STEP 1

Hakikisha kama simu yako ni model GT-I9505. Kama ni tofauti na hiyo tafadhali usiendelee unaweza ukaharibu simu yako.

STEP 2

Download Odin program zip file kwenye computer yako kwa kutumia link chini. http://www.mediafire.com/download/22oam83x98cxj8f/Latest_Odin3_v3.09.zip

STEP 3

Download TWRP kwa kutumia link chini kisha weka hilo file kwenye desktop
https://dl.twrp.me/jfltexx/twrp-2.8.6.0-jfltexx.tar

STEP 4

Unakumbuka lile file ulilo-download kwenye step2 (Odin zip file, Odin3 v3.09.zip)? sasa lifungue (Extract/Unzip) kwenye computer yako kwa kutumia (7-zip free software, au Win Rar) kisha liweke kwenye desktop pamoja na lile file ambalo umelidownload kwenye step 3 ambalo ni twrp-2.8.6.0-jfltexx.tar

STEP 5

Double-click the Odin3 v3.09.exe file to open Odin

STEP 6

Izime simu yako kisha subiri kama sekunde 10.Washa simu yako ya samsung galaxy S4 kwenye download mode. Tazama picha chini kisha soma maelekezo chini ya picha kujua jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode


Jinsi ya kuwasha simu yako kwenye download mode bonyeza kitufe cha katikati (Home) + cha kupunguza sauti (Volume down) + na cha kuwashia (power) kisha vishikilie kwa pamoja mpaka utakapoana kwenye screen yako maneno yanayosema Press Volume Up now to continue to Download Mode. Sasa achia halafu bonyeza cha kuongeza sauti. (Volume up) Hakikisha simu yako inamuonako kama picha ya kulia inavyoonyesha chini kabla ujaendele

STEP 7

Kwenye computer yako hakikisha uko kwenye ile Odin program ambayo uli double click kwenye step 4. Sasa chomeka simu kwenye computer ikiwa bado kwenye download mode kwakutumia usb cable. Odin itaitambua simu yako na itaonyesha message kama inavyoonekana kwenye picha chini

STEP 8

Kwenye Odin Click AP button na chagua lile file ambalo uli download kwenye step 2 ambalo uliliweka kwenye desktop. Jina la file ni twrp-2.8.6.0-jfltexx.tar

STEP 9

Muekano wako kwenye computer utakuwa hivi endapo utakuwa umenifwatilia vizuri. Tafadhali naomba Odin yako kwenye computer iwe na muonekano kama picha chini. Viboksi ambavyo vinatakiwa viwe na alama ya vema ni Auto Reboot na F.ResetTime kama inavyoonekana kwenye picha.

STEP 10

Kabla ya kuendelea hakikisha tupo pamoja. Usiendele kama ujaelewa.

STEP 11

Kwenye Odin bonyeza start button ambayo ipo chini kabisa kisha subiri mpaka utakapoana Odin imekuandikia PASS kama picha inavyoonyesha chini. Chomoa simu yako kwenye computer kisha subiri mpaka itakapowaka yenyewe kama ikichelewa kuwaka basi bonyeza cha kuwashia na itawaka kama kawaida.

STEP 12

Hongera mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako ya galaxy S4 (GT-I9505) na utakuwa na uwezo wa kuflash rom mbalimbali ili kupata muonekano mzuri na kuongeza ufanisi zaidi.

Endapo kama wewe ungependa uweke custom recovery kwenye simu yako na hauwezi basi wasiliana nasi kupitia namba +255684917346 na ghara itakuwa ni Tsh 25,000. Tu

No comments:

Post a Comment