Tuesday, June 30, 2015

JINSI YA KUPATA MUONEKANO MZURI KWENYE SIMU ZA ANDROID


Zipo njia nyingi sana za kubadili muonekano wa simu yako. Android inakuwezesha kubadili simu yako na kuifanya iwe jinsi unavyotaka iwe. Themes ni moja ya njia ambayo inatumika sana kwenye simu za android ili kubadili muonekano wa simu yako. Zipo baadhi ya simu ambazo zinakuja na app ya themes kama Samsung S6 na HTC M9. Asilimia nyingi ya simu za android haziji na hii application ya themes.



Njia ambayp inatumia na watu wengi kubadili muonekano wa simu za android ni icon packs. Icon Packs ni njia ambayo ipo maarufu sana hasa pale unapotaka kubadili application icon kwenye simu za android. Iride Ui ni icon pack inayokuwezesha kubadili icon zilizopo kwenye simu yako na kufanya simu yako iwe na muonekano wa kipekee

Note: Hii ni kwa watu wanaotumia simu ambazo zina android 5+

JINSI YA KUPATA MUONEKANO MZURI KWENYE SIMU ZA ANDROID


STEP 0

Download Apex Launcher kutoka kwenye playstore kisha install kwenye simu yako. Chagua apex launcher kama default launcher

STEP 1

Download Iride Ui kwa kutumia link chini kisha install kwenye simu yako
http://https://www.dropbox.com/s/8oy4joyvcbgv7il/Iride%20UI%20-%20Icon%20Pack%20v1.3.3.apk?dl=0

STEP 2

Bonyeza kisha sikilia icon ambayo unataka kubadilisha na utapata muonekano kama picha chini


STEP 3

Bonyeza kipengele cha edit kisha utapata muonekano kama picha chini


STEP 4

Bonyeza tena kile kialama unachotaka kukibadilisha na utapata muonekano kama picha chini


STEP 5

Chagua kipengele kinachosema select from icon packs kisha utapata muonekano kama picha chini


STEP 6

Chagua kipengele kinachosema Iride UI kisha sema ok na utaona icon tofauti tofauti. Chagua icon unayotaka kisha bonyeza tena sehemu iliyoandikwa ok

Kwa wale ambao hawana android 5, unaweza kutumia icon pack inayoitwa moonshine. Search kwenye play store kisha install kwenye simu yako kisha endelea kwanzia kwenye step 3.

Kwa wale wanaopenda blog yetu na wanataka tuendele zaidi basi usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment