Monday, August 31, 2015

JINSI YA KUTUMIA COMPUTER KUENDESHA SIMU YAKO YA ANDROID


Android inazidi kuwafurahisha watumiaji wa simu za android kila kukicha kwa kuifanya android izidi kuwa mbele daima. Sasa android imekuja na kitu kipya ambacho inakuwezesha kuiendesha simu yako kwa kutumia computer. Hii ni kweli na sio utani kwamba utaweza kuiamisha simu yako ya android na kuonekana kwenye computer na utaweza kutuma email, kucheza game, kutuma message na mambo mengine mengi kwa kutumia computer



JINSI YA KUTUMIA COMPUTER KUENDESHA SIMU YAKO YA ANDROID

STEP 0

Download android Usb drivers kwa kupitia link chini kisha install kwenye computer yako.
http://download.clockworkmod.com/test/UniversalAdbDriverSetup.msi

STEP 1

Nenda kwenye settings ya simu yako tazama kipengele kinachosema Developer Options kama picha inavyoonekana chini Note
Endapo Developer Options itakuwa haipo kwenye settings, nenda kwenye about phone kisha nenda kwenye kipengele kinachosema build number kisha ki bonyeze kama mara sita au saba kisha rudi tena kwenye settings halafu angalia kama developer options imetokea.





STEP 2

Ndani ya developer options hakiki ipo on na weka tick kwenye kipengele kinachosema Enable USB DEBUGGING kama picha inavyoonekana chini


STEP 3

Kwnye computer fungua browser ya chrome. Tembelea link chini kisha bonyeza kipengele kilichoandikwa ADD TO CHROME
https://chrome.google.com/webstore/detail/vysor-beta/gidgenkbbabolejbgbpnhbimgjbffefm?authuser=1


Endapo utafanikiwa utapata message kama yenye ujumbe kama picha chini


STEP 4

Baada ya hapo  nenda kwenye computer tafuta program inayoitwa chrome app launcher ambayo inakuwaga kwenye taskbar. Fngua chrome app launcher kisha click program inayoitwa vysor.

STEP 5

Chomeka usb cable kwenye simu yako na kwenye computer. Endapo utapata ujumbe kama picha chini kwenye simu yako, hakikisha unasema ok

Hapo hapo utaona kwenye computer yako simu yako imeunganishwa na utapata ujumbe kama picha inavyoonekana chini kwenye simu yako



Kwa wale wanaopenda kazi zetu mnaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment