Wednesday, September 2, 2015

SHARE PICHA NYINGI KWA WAKATI MMOJA KWA KUTUMIA GOOGLE PHOTOS


Zipo njia nyingi za kushare picha kwenye simu za android. Moja ya njia ambayo inatumika kushare picha nyingi kwa wakati mmoja ni whatsapp, Gmail etc. Tatizo linakuja pale unapotaka ku share picha nyingi. Mfano unataka ku-share picha 40 kwa wakati mmoja, itakuwia vigumu kutumia whatsapp au gmail.



Leo tutaona jinsi ya ku-share picha nyingi zaidi ya hata 40 kwa wakati mmoja kwa kutumia google photos. Google Photos ni app kutoka Google ambayo inakuwa uwezo mkubwa pale unapotaka kufanyia kazi picha na video zako. Zipo faida nyingi sana za Google Photos.

JINSI YA KU-SHARE PICHA NYINGI KWA WAKATI MMOJA KWA KUTUMIA GOOGLE PHOTOS

STEP 1

Cha kwanza kabisa haikikisha umeweka app ya google photos kwenye simu yako. Kama bado tembelea link chini ili uweze kuweka google photos kwenye simu yako
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.apps.photos&hl=en

STEP 2

Fungua Google Photos Chagua picha zote ambazo unataka ku-share na mwenzako. Tazama picha chini kuelewa zaidi


STEP 3

Juu kabisa utaona ile alama ya share. Bonyeza alama ya share utapata muonekano kama picha chini


STEP 4

Bonyeza sehemu iliyoandikwa Get Link utapata muonekano kama picha chini


STEP 5

Subiri wakati google photos ikiwa ina upload picha zako.

STEP 6

Baada ya kumaliza uploading, itakuandikia getting a link


STEP 7

Nenda kwenye whatsapp au message kisha shikilia sehemu ya kuandikia ujumbe mpaka uone neno linasema paste. Baada ya hapo rafiki yako atapata link ambayo akibonyeza itafungua website na ataweza kuona picha zote ulizomtumia kama picha chini inavyoonekana



STEP 8

Endapo rafiki yako atataka kuzichukua hizo picha atabidi abonyeze vidoti vitatu juu kabisa na utapata muonekano kama picha chini.


STEP 9

Atabonyeza kipengele kinachosema Select kisha atachagua picha zote anazotaka kuzichukua na atapata muonekano kama picha chini


STEP 10

Juu kabisa atabonyeza alama yenye mawingu na mshale wa kusha chini na atakuwa amefanikiwa ku-download picha ambazo umemtumia.

Kwa wale wanaopenda kazi zetu mnaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment