Saturday, September 19, 2015

JINSI KUIBADILISHA ICONS ZA TECNO BOOM J7 ZIFANANE NA SAMSUNG GALAXY NOTE 5


Tecno Boom J7 ni simu iliyochukua umaarufu mkubwa kwa kuwa na uwezo wa kupiga music kwa kupitia earphones huku ikiwa na android 4.4.4. Tatizo moja kubwa la simu za Tecno ni updates. Tecno wanachelewa au hawatoi kabisa updates za simu zao kama ilivyo kwenye simu nyingine kama Samsung, HTC, Sony na LG.



Kutoka na hilo tatizo watu wengi wenye simu za Tecno hukimbilia kwenye custom rom. Leo tutaona jinsi ya kubadilisha muonekano wa Tecno Boom J7 ufanane kidogo na Samsung Galaxy NOTE 5. Vitu ambavyo tutafanya ni kubadilisha icon za Boom J7 ziwe kama Note 5 na kuweka Widget ya S6.

JINSI KUIBADILISHA TECNO BOOM J7 IFANANE NA SAMSUNG

STEP 1

Download Es File Explorer kutoka kwenye play store. Unaweza tumia link chini kudownload Es File Explorer kisha install kwenye simu yako
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.estrongs.android.pop&hl=en

STEP 2

Download icon za Samsung Galaxy S6 kwa kutumia link chini kisha zi extract na uziweke kwenye folder ndani ya simu yako
https://mega.nz/#!K0J3kJba!uzBQp3tXX...7BLGF2KXo6NZfM

STEP 3

Install Nova Launcer au Apex launcher kutoka kwenye Playstore. Mimi binafsi napendelea Apex Launcher

STEP 4

Kwa kutumia apex launcher au nova launcher nenda kwenye apps kisha chagua app ambayo unataka icon yake ifanane na Samsung Galaxy S6.
Mfano mimi nimechagua icon ya video, shikilia icon ya video kisha ipeleke mpaka sehemu iliyoandikwa Edit kisha utaona muonekano unaofanana na picha chini


STEP 5

Bonyeza  Icon ya video  kisha utaona muonekano kama picha chini


STEP 6

Chagua select picture. Kisha utaona muonekano kama picha chini


STEP 7

Bonyeza kipengele kilicho andikwa Es File explorer kisha nenda kachague lile folder ambalo uliweka icons ambazo uli download kwenye step 2. Kama umesahau rudia tena step 2

STEP 8

Kisha chagua icon ya video kisha bonyeza ok. Ukitaka kubadilisha Icon nyingine rudia tena kama ulivyofanya kwenye icon ya video

STEP 9

Endapo utataka kuweka Weather Widget kama Galaxy S6, Tembelea link chini kujua jinsi ya kuweka weather widget kama ya S6
http://phonetricktz.blogspot.com/2015/05/jinsi-ya-kuweka-weather-widget-ya.html

Kwa wale wanaopenda kazi zetu mnaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

2 comments:

  1. Replies
    1. Yes unaweza badilisha.. fwatilizia maelezo hayo hayo kwenye h6

      Delete