Sunday, October 18, 2015

ANDROID 6.0 (MARSHMALLOW), KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA?

Toleo la kwanza kabisa la android ni Android 1.6 (Donut), baada ya hapo ikaja Android 2.1 (Eclair), halafu inayofwata ni Android 2.2 (Froyo) ambayo ndio ilianza kuipa umaarufu simu za android. Baada ya hapo ikaja Android 2.3 (Gingerbread) halafu Android 3.0 (Honeycomb). Toleo la android 3.0 halikufanya vizuri sana na kusababisha google kutoa toleo lingine mdaa mfupi Android 4.0 (Ice Cream Sandwich) na hapo hapo android ili rudi tena kwenye chart.



Tolea lilofwata ni Android 4.1 (Jelly Bean) kisha ikaja Android 4.4 (Kitkat) ambayo kwa sasa ndio inayo tumiwa na watu wengi kushinda toleo lolote lile la android. Google hawakuishia hapo baadae kidogo walikuja na toleo ambalo lilisifika sana kwa sababu lilibadilisha mfumo mzima wa android na kuwa material design na kubatizwa jina la Android 5.0 (Lollipop).

Leo tutaongelea toleo jipya kabisa la android ambalo ni Android 6.0 (Marshmallow). Toleo hili limetoka miezi michache iliyopita na limekuja na vitu tofauti tofauti ambavyo havikuwepo kwenye matoleo ya android yaliyopita.

Moja ya kitu kikubwa ambacho kinasifiwa na watu wengi ambacho kipo kwenye Android 6.0 (Marshmallow) ni Now on Tap. Kwa kifupi Now on Tap inakurahisishia kupata habari zaidi ya kitu ambacho unakisoma kwenye screen yako. Kwa mfano, mtu amekutumia ujumbe wa whatsapp akiwa anakwambia utazame movie inayoitwa Mad Max Fury Road. Hapo ndipo now on tap inapokuja, ukishikilia kitufe cha home button, now on tap itajaribu kusoma screen yako na kukupa habari zaid kuhusu Mad Max Fury Road kama nani ni Actor, inaonyeshwa kwenye cinema gani na mambo mengine mengi

Kitu kingine cha msingi ni App Permission. Android 6.0 (Marshmallow) inakupa uwezo zaidi wa kuingoza simu yako kama kuruhusu au kukataa baadhi za apps zisiwezi kuchukua information kama contact au kuzikataza app zisiweze kutumia data kwenye simu yako. Kwa wale ambao hawapendi data itumike haraka basi android marshmallow ndio sulihisho

Tazama video chini kuendelea kujua mambo mengine ambayo yapo kwenye android (Marshmallow)

Kwa sasa simu ambayo inatumia Android 6.0 ni Nexus 6p na 5x. Wengi wetu tukiwa tunasubiri makampuni kama Samsung, HTC, lG na Sony watoe updates ambazo zitafanya simu zao zitumie Android 6.0. Kwa wale wanao tumia simu za Tecno kiukweli mtasubiri sana kupata mabadiliko

Endapo ungependa kusaidiwa ku update simu yako na uweze kutumia angalau android 5.0 na kuendelea basi unaweza kututafuta kwenye instagram kupitia phonetricktz au kwenye facebook yetu iliyo pembeni kulia au unaweza ku comment chini na utajibiwa

No comments:

Post a Comment