Keyboard ambayo inatumika kwenye sony xperia smartphone sasa pia inaweza kutumika kwenye simu za kichina kama Tecno Boom j7. Moja ya kitu kinachovutia kwenye hii sony xperia keyboard ni kuwa na muonekano unaofanana na ule kutoka Samsung.
Tusiongee maneno mengi sana, sasa twende tuangalie jinsi ya kuweka sony xperia keyboard kwenye Tecno Boom J7.
JINSI YA KUWEKA KEYBOARD YA SONY XPERIA KWENYE TECNO BOOM J7
Vigezo na Masharti
- 1: Hakikisha simu yako ni Tecno Boom J7
- 2: Hakikisha tayari simu yako imekuwa rooted
- 3: Hakikisha umeweka custom recovery kwenye simu yako
- 4: Hakikisha unafanya backup ya simu yako ili kuwa kwenye upande wa usalama zaidi
- 5: Mimi sitausika kwa chochote endapo utashindwa kufwata malekezo na kuaribu simu yako
STEP 0
Hakikisha tayari umeweka custom recovery kwenye tecno boom j7. Kama bado tembelea link chini kujua jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Tecno Boom j7http://phonetricktz.blogspot.com/2015/10/jinsi-ya-kuweka-custom-recovery-kwenye.html
STEP 1
Download Sony xperia keyboard kwa kutumia link chini kisha weka hilo file ndani ya memory card yako na hakikisha hauliweki ndani ya folder lolote.http://forum.xda-developers.com/attachment.php?attachmentid=3429696&d=1438819844
STEP 2
Zima simu yako kisha iwashe kwenye recovery mode.Note
Ili kuwasha Tecno Boom J7 kwenye recovery mode, zima simu yako kisha bonyeza cha kuwashia na kuongeza sauti kwa wakati mmoja na uvishikilia mpaka simu yako itakapoonyesha picha kama chini kisha uachie. Unaweza kutumia cha kupunguza sauti kama muongozo na cha kuwashia kama kutekeleza ulichochagua.
STEP 3
Nenda kwenye kipengele kinachosema install zip kama picha inavyo onekana chini kisha bonyeza cha kuwashiaSTEP 4
Nenda kwenye kipengele kinachosema choose zip from sdcard kama picha inavyo onekana chini kisha bonyeza cha kuwashiaSTEP 5
Shuka chini kabisa kisha chagua lile file ambalo uli download kwenye Step 1 kisha ukaliweka kwenye memory card yako kisha bonyeza cha kuwashiaSTEP 6
Nenda hadi kwenye kipengele kinachosema Yes kama picha chini kisha bonyeza cha kuwashia. Simu yako ita install sony xperia keyboard na utaona ujumbe umesema completeSTEP 7
Washa simu yako kisha nenda kwenye settings za simu yako kama picha chiniSTEP 8
Nenda kwenye kipengele kinachosema language and input na hakikisha kipengele kinachosema xperia keyboard kinakuwa na alama ya vema kama picha chini,STEP 9
Kisha bonyeza kipengele kinachosema default kisha chagua kipengele kinachosema International keyboard (xperia keyboard) na utapata muonekano kama picha chiniSTEP 10
Baada ya hapo bonyeza vile vialama ambavyo vipo pembeni ya neno xperia keyboard kama picha chiniSTEP 11
Bonyeza kipengele kinachosema personalization guideSTEP 12
Kisha chagua neno linalosema i never want to have any words or letters replaced kama picha chini. Chini kabisa bonyeza kialama kinacho ashiria kwenda mbeleSTEP 13
Chagua language unayotaka mfano English (US) kisha download dictionary yake baada ya hapo chini kabisa bonyeza kialama kinacho ashiria kwenda mbeleSTEP 14
Hakikisha numeric keys ipo on ili kuwa na mstari wa namba kwenye keyboard yakoMpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka na kutumia xperia keyboard yenye mstari wa number kama ilivyo kwenye simu za Samsung.
Kama umependa kazi yetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz
No comments:
Post a Comment