Saturday, October 31, 2015

CAMERA MBILI BORA UNAZOWEZA KUTUMIA KWENYE KILA SIMU YA ANDROID

Camera ni moja ya kitu kinachovutia sana kwenye smartphone. Smartphone isipokuwa na camera nzuri hupelekea kupoteza mvuto wake na hata kusababisha kampuni ya simu kupoteza mauzo

Leo tutachambua camera tatu bora ambazo unaweza kuziweka kwenye simu yako ya android na kukufanya ufurahie picha unazopiga pamoja na video.

Google Camera

Note : Google Camera inatumika tu kwenye simu zenye android 4.4 na kuendelea

Wengi tunatumia simu za android na kusahau kama google wanayo camera yao ambayo inaitwa Google Camera. Moja ya sifa ya hii camera ni muonekano wake pamoja na ubora wa picha na video bila kusahau uwepesi wake wa kutumika hata kwenye zile simu ambazo zina uwezo mdogo.

Baadhi ya mambo mazuri yanayo patikana kwenye Google Camera ni Easy Interface, Lens Blur, HDR+ (High Dynamic Range + Low Light){kukuwezesha kupata picha nzuri kwenye sehemu ambazo hazina mwanga, Photo Stitching, Android Wear (kukuwezesha kupiga picha kirahisi kwa kutumia saa ya android). Unaweza download Google Camera kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.GoogleCamera&hl=en

Picha chini zinaonyesha muonekano wa Google Camera

HTC M9 CAMERA

Hapo utakuwa unajiuliza maswali kama naweza vipi kutumia camera ya HTC kwenye simu aina tofauti na HTC? Jibu ni kwamba inawezekana kwa maana hii camera tayari imefanyiwa marekebisho na watundu na sasa utaweza kuitumia kwenye Samsung, Sony, Tecno, Huawei, LG etc

HTC M9 Camera ina mambo mazuri kama Photo Booth, Split Capture, Bokeh, Selfie, Camera, Panorama. Unaweza donload htc m9 camera kwa kupitia link chini
https://mega.nz/#!9ERX0aLQ!E2f5FJ9KafQTkvk3S75BqAYx9HMMXbbrb2M3X0ugVGw"

Baada ya kumaliza ku download fungu hilo file ulilo download kisha install camera pamoja na gallery kisha zima na kuwasha simu yako.Picha chini zinaonyesha muonekano wa HTC M9 Camera







Mpaka hapo tumefika mwisho. Kama umependa kazi yetu unaweza ukatufwata kwenye intagram kwa kutumia phonetricktz

No comments:

Post a Comment