Monday, November 2, 2015

JINSI YA KUZUIA APPS KWENYE SIMU ZA ANDROID ZISIWEZE KUTUMIA DATA

Zipo apps nyingi sana kwenye simu za android ambazo zinahitaji kutumia data (internet) ili ziweze kufanya kazi. Kabla ya android 5.0 (lollipop) kuanzishwa watumiaji wa simu za android walikuwa inawalazimu ku root simu zao ili waweze kuzuia baadhi ya apps zisiweze kutumia data.

Kwa kutumia app inayoitwa NetGuard utaweza kuzuia apps zisiweze kutumia internet. Kwa mfano unataka kutumia internet kucheck youtube lakin mdaa huo huo hutaki message za whatsapp au facebook kukuingilia hapo ndipo NetGuard inapousika.

Kwa kifupi haina haja ya kuzima data ili usionekane whatsapp unachotakiwa kufanya ni kuifungia whatsapp peke yake ili isiweze kutumia data mpaka utakapoamua kuirudisha iendelee kutumia data.

Faida za NetGuard ni kupunguza matumizi yako ya data, kuifanya battery ya simu yako iweze kukaa mda mrefu na kukupa uwezo wa kufanya mambo yako bila kuingiliwa (privacy).
Kwa sasa NetGuard inafaa kwa wale wanao tumia android 5.0 na kuendelea. Kama simu yako inatumia android chini ya hapo basi hautaweza kutumia NetGuard

Unaweza donwload NetGuard kwa kutukia link chini kisha install kwenye simu yako
https://github.com/M66B/NetGuard/releases/download/0.13/NetGuard-v0.13.apk

Kwa mfano ukitazama picha chini utaweza kugundua kwamba whatsapp tu ndio ina ruksa ya kutumia mobile data kwenye simu yangu lakin haina ruksa ya kutumia Wi-Fi
Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama unataka kuendelea kujua mambo mengi kuhusiana na android usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment