Wednesday, November 11, 2015

JINSI YA KUWEKA BLACKBERRY PRIV KEYBOARD KWENYE SIMU ZA ANDROID

Siku chache zilizopita Blackberry wali itambulisha simu yao ya kwanza (Blackberry Priv) ambayo itakuwa inatumia mfumo wa Android. Blackberry Priv tayari ipo madukani huko America pamoja na Ulaya.

Kwa wale ambao hawataki kusubiri mpaka Blackberry Priv itue Africa, sasa unaweza kuendelea kupata au kutumia baadhi ya vitu vichache ambavyo vipo kwenye Blackberry Priv kama Keyboard, Contacts na Launcher.

Leo tutajifunza jinsi ya kuweka Blackberry Priv keyboard kwenye simu yako ya android. Hii keyboard inafanya kazi kwenye simu ambazo zinatumia android 5 na kuendelea.

Step 0

Download Blackberry Priv Keyboard kwa kutumia link chini, kisha install kwenye simu yako.
https://mega.nz/#!Rp9CQYJI!v8Nocl5asKxDw4XconKOW1Pu3j5CNd0Ocq7xXVVvAMg

Step 1

Baada ya kumaliza ku-install bonyeza sehemu iliyoandikwa open na utapata muonekano kama picha chini

Step 2

Bonyeza sehemu iliyoandikwa get started kisha utaona muonekano kama picha chini

Step 3

Bonyeza sehemu iliyoandikwa enable in settings kisha utaona muonekano kama picha chini

Step 4

Weka tick kwenye kibox cha Blackberry keyboard kisha bonyeza ok na utapata muonekano kama picha chini

Step 5

Bonyeza sehemu iliyoandikwa switch input method kisha utaona muonekano kama picha chini

STEP 6

Chagua BLackberry Keyboard kama default Keyboard kisha bonyeza finish.




Picha chini zinaonyesha muonekano wa Blackberry Priv Keyboard kwenye simu yangu









Mpaka hapo tumefikia mwisho na kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz

No comments:

Post a Comment