Friday, January 29, 2016

JINSI YA KUTOA LUGHA YA KICHINA KWENYE MPESA MENU, TIGO PESA NA MENU YA KUJIUNGA NA KIFURUSHI

Zipo baadhi ya simu za android ambazo huwa zinaleta lugha ya kichina au kijapani pale unapopiga namba za Mpesa (*150*00#) au Tigo pesa au pale unapotaka kujiunga na kifurushi. Tatizo hili hutokea sana kwenye simu zinazotumia mfumo wa android.

Sababu kubwa inapolekea kupata lugha ya kichina au kijapani pale unapo jaribu kupiga ussd code kama ya Mpesa au Tigo pesa ni modem zilizopo kwenye simu yako. Simu zilizo tengenezwa kwa ajili ya nchi kama china au japan huwa zinawekewa modems ambazo hupelekea kukumbana na tatizo kama hili.

Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanakutana na hili tatizo unachotakiwa kufanya ni kubadilisha modems za simu yako. Usijidanganye ku factory reset maana hautafanikiwa kutatua hilo tatizo. Kwa wale ambao wamekutana na tatizo kama hili basi cha kufanya ni kuflash simu yako upya na firmware nyingine.

Kama ungependa kupata msaada wa kutatua tatizo hilo basi unaweza wasiliana nasi kupitia namba +255753877552. Gharama isiyopungua Tsh 30,000/= utatakiwa kulipa.

Kama unapenda kazi zetu unaweza ukatufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment