Thursday, May 19, 2016

GOOGLE WAZINDUA APPS MBILI MPYA, ALLO PAMOJA NA DUO

Tamasha kubwa linalo andaliwa na Google kila mwaka Google I/O lilifanyika jana likiwa linalenga mambo muhimu ambayo Google wanatarajia kuanzisha, mambo mapya yatakayo kuwepo kwenye android pamoja na vifaa vipya ambavyo google wanatarajia kuvianzisha.

Hili tamasha hurushwa live kupitia youtube ili hata mimi au wewe ambao tunaishi huku AFRICA tusipitwe na mambo mazuri ambayo Google wanatarajia kuyaleta kwenye maisha yetu.

Moja ya vitu ambavyo Google walizindua jana ni application mbili ambazo zitakuja kwenye android siku chache zijazo. Moja ya application ambayo iliwavutia watu wengi sana na kuwaacha midomo wazi ni Allo.

Allo ni chatting application kama ilivyo Whatsapp lakin hii ipo kipekee kabisa na itakuwa mpinzani mkubwa wa Whatsaap. Moja ya sifa kubwa ya hii app ni kupunguza muda wa ku type kwa kukupa smart reply. Mfano mtu akikikutumia picha ya mbwa, hii app ina uwezo wa kujua hiyo picha iliyotumwa ni kitu gani na inakupa reply za kuchagua kama nice dog, ugly dog etc.

Kitu kingine kizuri kuhusu Allo ni kuwa integrated (kuchanganywa) na Google Assistant. Hii ina maanisha kwamba ukiwa unatumia hii app na unataka ku search kitu kwenye google basi utaweza kufanya hapo hapo ukiwa ndani ya hiyo app. Hii ni tofauti kabisa na apps nyingine kama Whatsapp ambazo inakubidi utoke kwenye whatsapp uende kwenye google search halafu urudi tena kwenye whatsapp...mambo ya kizamani hayo...

Tazama video tatu fupi chini zinazo onyesha jinsi Allo inavyo fanya kazi.







Duo ni app nyingine ambayo pia ilizinduliwa jana. Duo ni video calling app kama ilivyo Skype au Viber. Duo app pia ipo kipekee kabisa ukilinganisha na apps nyingine za video calling au video chatting. Sifa moja kubwa ya Duo ni knock knock. Mfano mtu akiwa anakupigia video call, basi utaweza kumuona huyo mtu anayekupigia anafanya nini hata kabla hujapokea simu yake...hahaaaaaaaaa.... hatari... kama huamini check video chini



Kwa wale ambao walikosa jana basi unaweza kutazama video chini ambayo inaelezea mambo matano makubwa yaliyo yambulishwa na Google



Mpaka hapo tumefikia mwisho, kwa wale wanaopenda kutufutwa kwenye instagram utatupata kupitia phonetricktz.

No comments:

Post a Comment