Thursday, September 22, 2016

GOOGLE ALLO, MPINZANI WA WHATSAPP

Google Allo ni app mpya ya kuchat kutoka Google ambayo ipo kijanja (ki-smart) zaidi kushinda mitandao menginge ya kuchat kama whatsapp, messenger, Tango, Tellegram. Baada ya Google kuona hawafanyi vizuri kwenye apps za kuchat basi wameamua kujipanga na kuzindua Google Allo

Kwa kifupi Google Allo imekuja na mambo mengi sana, moja wapo ni uwezo wa kutumia google assistant ukiwa kwenye Google Allo. Hii ina maanisha sasa una uwezo wa ku-search google ukiwa ndani ya app au una uwezo wa ku-book ticket za movies bila hata ya kutoka kwenye Google allo.

Jambo lingine lipya lilipo kwenye Google Allo ni smart reply. Kwa mfano mtu akikutumia picha ya mbwa wakati mnachat, Google Allo inauwezo wa kutumbua hiyo picha iliyotumwa ni ya Mbwa halafu ikakupa sentence za kumjibu mwenzako kama Nice Dog, cute dog. Hii ina saidia sana kukupunguzia mdaa wa ku-type... hahaaaaa

Google Allo pia inakuja na Emoji nyingi sana ambazo hazipo kwenye mitandao mengine ya Kuchat kama Whatsapp au Messenger. Pia una uwezo wa ku-edit picha ukiwa kwenye Google allo halafu ukamtumia rafiki yao.

Tazama video chini kuona mambo mengine yaliyopo kwenye Google Allo



Kwa wale wanaotaka kujaribu Google Allo leo basi unaweza ku-download kutoka kwenye playstore kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.apps.fireball&hl=en

Kama link juu haifanyi kazi basi unaweza download kwa kutumia link chini
http://www.apkmirror.com/apk/google-inc/allo-by-google/allo-by-google-1-0-006_rc18-release/

Kwa umependa kazi zetu, unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia Phonetricktz

No comments:

Post a Comment