Saturday, September 24, 2016

TOFAUTI KATI YA GOOGLE ALLO NA WHATSAPP

Whatsapp ilianza kutumika kwenye smartphones mbalimbali kuanzia mwaka 2009. Kitu kimoja kilichosaidia whatsapp kuweza kupata umaarufu kwa haraka ni uwezo wake kutumika kwenye smartphone tofauti tofauti (cross-platform). Hii ina maanisha kwamba whatsapp ilikuwa inapatikana kwenye simu za Nokia, Android, Blackberry OS, pamoja na IOS (Iphone).

Google Allo ni mtandao mpya ambao ulizinduliwa na Google May 2016 na matumizi yake hayana tofauti sana na whatsapp. Google Allo imepewa jina la smart messaging app kwa maana ni mtandao wa kuchat ambao upo kipekee na wenye uwezo wa kufikiri mambo kutoka na wewe unavyotaka.

Moja ya tofauti kubwa kati ya Google allo na Whatsapp ni kwamba Google allo ina Google assistant ndani yake wakati whatsapp haina. Google assistant ina iwezesha Google allo kuweza kufanya mambo kama Google search, Booking for Movie Tickets, huku ukiwa unachat na rafiki yako. Ina maanisha kwamba ukiwa na Google allo hauna haja ya kwenda kwenye Google search halafu urudi tena kwenye google allo. Vitu vyote unaweza ukavifanyia ndani ya Google Allo.

Tofauti nyingine kubwa kati ya Whatsapp na Google allo ni Smart reply. Google allo inakuja na smart reply. Smart reply ina maanisha nini? Mfano tazama picha chini. Watu wawili wana chat na mmoja kamtumia mwenzake picha. Chini ya picha tayari Google allo imeshaichunguza hiyo picha na ina kupendekezea maneno ya kumjibu kama so brave, How exciting , How fun.



Kwa hiyo kama unataka kujibu so brave huna haja ya ku-type una bonyeza tu hapo panaposema so brave.. Google allo ina tupunguzia muda wa kuanza ku-type..

Google allo pia inakuja na powerful picture editing. Kwa wale wanaopenda ku-edit picha zao basi ukiwa na google allo ndio umefika nyumbani. Hii ina maanisha kwamba wewe huna haja ya kutafuta app ya ku-edit picha halafu ukimaliza ku-edit picha umtumie rafiki yako labda kwa kutumia whatsapp, kwenye google allo mambo yote hayo unaweza kufanyia humo humo ndani ya google allo.

Sio kwamba Google allo ina mambo mengi kushinda whatsapp, Mfano Whatsapp ina mambo kama Whatsapp for Web..Mimi binafsi napenda sana kutumia whatsapp for web. Hii huwa inanipunguzia mdaa wa kuchukua simu yangu wakati nikiwa kwenye laptop na kuanza kujibu zile message za ma-group. Whatsapp for web inakuwezesha kutumia whatsapp ukiwa kwenye computer yako. Google allo haina mambo kama hayo

Google allo pia haina uwezo wa kukwambia mshikaji wako au demu wako alionekana online saa ngapi? hahahhaaaaaaaaaaaaa... Kwenye whatsapp mambo kama hayo yanawezekana. Kitu kingine kizuri kuhusu Google allo ni stickers. Google allo inakuja na stickers nzuri ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako, mfano tazama picha chini



Hizo ni baadhi ya tofauti zilizopo kati ya Google allo na Whatsapp. Mimi binafsi nadhani whatsapp na Google allo zote zipo vizuri na zote mimi natumia. Lakini sidhani kama Google allo itakuja kuwa maarufu kama whatsapp. Kwa wale wanaotaka kujaribu Google allo basi tembelea link chini ili uweze ku-download na kuijaribu kwenye simu yako
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.apps.fireball&hl=en

Msiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz ili kuweza kujua mengi kuhusu android.

No comments:

Post a Comment