Samsung Galaxy Grand Prime (SM-G530H) ni simu yenye uwezo wa kutumia line mbili huku ikiwa na android kitkat(4.4.4) na pia unaweza ku-update hadi kufikia android 5.0.2. Ku root hii simu siyo rahisi kama ilivyo kwenye matoleo mengine ya Samsung. Endapo utakosea ku root hii simu basi unaweza kuaribi simu yako na kukusababishia harasa kubwa.
Maelekezo niliyo yatoa chini ni kwa ajili ya Samsung Galaxy Grand Prime (SM-G530H) tu. Usije jaribu kutumia maelekezo haya kwenye aina nyingine ya samsung.
https://drive.google.com/file/d/0B2FZbKKFAr42X2ZpY0FNRjlIMkk/view?usp=sharing
Note
Hakikisha program yako ya odin ina fanana na picha juu kwa zaidi ya asilimia 98%. Haikisha vitiki kwenye program yako ya odin vina fanana na vyangu kisha subiri kama dakika 1
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa ku-root Samsung Galaxy Grand Prime (SM-G530H), kama una shida yeyote kuhusiana na hii simu unaweza wasiliana nasi kupitia whatsapp +255627732383.
Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ambayo ni phonetricktz au unaweza like facebook yetu.
Maelekezo niliyo yatoa chini ni kwa ajili ya Samsung Galaxy Grand Prime (SM-G530H) tu. Usije jaribu kutumia maelekezo haya kwenye aina nyingine ya samsung.
JINSI YA KU ROOT SAMSUNG GALAXY GRAND PRIME (SM-G530H)
Vigezo na Masharti
- 1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
- 2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer
- 3: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy Grand Prime (SM-G530H)
- 4: Computer inayotumia Window
STEP 0
Download Root_grand_prime_sm-g530h-mohan.zip kwa kutumia link chini kisha lifungue hilo file na ndani yake utakuwa na mafile kama kwenye picha chinihttps://drive.google.com/file/d/0B2FZbKKFAr42X2ZpY0FNRjlIMkk/view?usp=sharing
STEP 1
Zima simu yako kisha iwashe kwenye download mode. Kama ujui jinsi ya kuwasha simu kwenye download mode unachotakiwa kufanya ni zima (turn off) simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kupunguza sauti(vol down button)} na cha kuwashia (power button) mpaka simu itakapowaka kama picha inavyo onekana chini ndipo uachie vitufe vyote kwa pamoja.STEP 2
Bonyeza kitufe cha kuongeza sauti kwenda kwenye Download Mode na utapata muonekano kama picha chini. Endapo una wasiwasi kwamba simu yako itaaribika au unaogopa na unataka simu yako irudi kama kawaida basi bonyeza kitufe cha kupunguza sauti au toa battery kisha rudishia kisha washa simu yako. Kama wewe hugopi na unataka kuendelea basi endelea kufwatilizia maelekezoSTEP 3
Ndani ya lile file(folder) ulilolipata kwenye Step 1, fungua program inayoitwa Odin3-v3.10.6.exe kisha utapata muonekano kama picha chiniSTEP 4
Chukua USB kisha chomeka kwenye simu yako ya Galaxy Grand Prime SM-G530H halafu chomeka kwenye computer kisha kwenye program ya odin utaona kibox kinarangi kimeandikwa com(xx) na neno linalosema added kama picha chiniSTEP 5
Kwenye program yako ya Odin bonyeza kipengele kinachosema Ap ambacho kipo kulia kisha utaona window mpya imefunguka. Kwa kutumia hiyo window iliyofunguka chagua lile file linaloitwa 2_cache_recovery_stock_mohan_sm-g530h.tar ambalo uli download kwenye Step 0 kisha bonyeza open. Endapo utafanikiwa basi program yako ya odin itafanana na kama yangu kwenye picha chini.Note
Hakikisha program yako ya odin ina fanana na picha juu kwa zaidi ya asilimia 98%. Haikisha vitiki kwenye program yako ya odin vina fanana na vyangu kisha subiri kama dakika 1
STEP 6
Chini kwenye program yako ya Odin, bonyeza kipengele kinachosema Start kisha subiri mpaka utakapona program yako ya Odin imesema neno Pass na ina muoenakano kama picha chini. Kisha simu yako itazima na kujiwasha yenyewe.STEP 7
Simu yako itazima na kujiwasha. Chomoa USB yako kutoka kwenye computer. Ifunge program ya odin kwenye computer yako, kisha washa tena simu yako kwenye download mode kama ulivyofanya kwenye STEP 1 na STEP 2, kisha ifungue tena program ya odin kama ulivyofanya kweye STEP 3. Chukua USB kisha chomeka kwenye simu yako ya Galaxy Grand Prime SM-G530H kisha utapata muonekano kama kwenye picha iliyopo kwenye STEP 4.STEP 8
Kwenye program yako ya Odin bonyeza kipengele kinachosema Ap ambacho kipo kulia kisha utaona window mpya imefunguka. Kwa kutumia hiyo window iliyofunguka chagua lile file linaloitwa 1_cfroot_sm-g530h_mohan.tar ambalo uli download kwenye Step 0 kisha bonyeza open. Endapo utafanikiwa basi program yako ya odin itafanana na kama yangu kwenye picha chini.STEP 9
Chini kwenye program yako ya Odin, bonyeza kipengele kinachosema Start kisha subiri mpaka utakapona program yako ya Odin imesema neno Pass na ina muoenakano kama picha chini. Kisha simu yako itazima na kujiwasha yenyewe.STEP 10
Simu yako itazima na kujiwasha. Chomoa USB yako kutoka kwenye computer. Baada ya simu yako kuwaka ndani utaona app ya super user. Ifungue kisha utapata ujumbe unaosema Disable Knox. Sema ok, kisha subiri. Baada ya hapo utapata ujumbe mwingine unaosema Instal scripts, chagua Normal.Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa ku-root Samsung Galaxy Grand Prime (SM-G530H), kama una shida yeyote kuhusiana na hii simu unaweza wasiliana nasi kupitia whatsapp +255627732383.
Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ambayo ni phonetricktz au unaweza like facebook yetu.
No comments:
Post a Comment