Friday, September 16, 2016

JINSI YA KU UPDATE SAMSUNG GALAXY S4 KUWA KAMA GALAXY NOTE 5

Samsung Galaxy S4 ni moja ya simu nzuri sanaa kwa kuwa na uwezo mkubwa hata kuweza kumkaribia mkubwa wake Galaxy S5. Uzuri wa Samsung Galaxy S4 unaongezeka pale utakapo weke custom rom na kuifanya iwe na muonekano wa kijanja kama ilivyo Note 5

Leo tutajifunza jinsi ya kuweka custom rom kwenye Galaxy S4 (GT-I9505) na kuifanya iwe na muonekano kama Galaxy Note 5.

Vigezo na Masharti vya kuzingatia

  • 1: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako.
  • 2: Hakikisha unauelewa kidogo wa computer
  • 3: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy S4 GT-I9505
  • 4: Uzoefu wa ku-flash custom rom unaitajika

JINSI YA KU UPDATE SAMSUNG GALAXY S4 KUWA KAMA GALAXY NOTE 5

STEP 0

Hakikisha tayari umeweka custom recovery kwenye simu yako ya S4 GT-I9505. Kama bado unaweza kujifunza jinsi ya kuweka custom recovery kwenye S4 GT-I9505 kwa kupitia link chini
http://phonetricktz.blogspot.com/2015/07/jinsi-ya-kuweka-custom-recovery-kwenye.html

STEP 1

Update modem ya simu yako kwa kusoma maelekezo yaliyopo kwenye link chini. Usipo update modem basi utaweza kutumia WiFi.
http://forum.xda-developers.com/showpost.php?p=62593102&postcount=5402

STEP 2

Download Albe95 LolliROM 9.0 kwa kutumia link chini kisha lihifadhi hilo file kwenye memory card ya simu yako
https://mega.nz/#!Wg5gzZ6Q!Fb_oX_PK1zk5WFAgTj-1TrzXge0IfvV3trfv6El1_T0

STEP 3

Zima simu yako, kisha washa simu yako kwenye recovery mode. Kwa wale ambao hawajui jinsi ya kuwasha simu kwenye recovery mode soma maelekezo chini

Zima simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuwashia (power button) na cha kuongeza sauti(vol up button)} mpaka simu itakopo onyesha logo ya Samsung kisha viachie vitufe kwa pamoja.

Endapo utafanikiwa utapata muonekano kama picha chini

STEP 4

Bonyeza kipengele cha Backup, halafu hakikisha una backup simu yako ili uweze kuirudisha kama ilivyokuwa endapo simu yako itakapo leta shida baada ya kueweka Albe95 LolliROM 9.0

STEP 5

Baada ya kumaliza ku backup, nenda kwenye kipengele cha wipe kisha swipe to factory reset ili kufuta vitu vyote kwenye simu yako.

STEP 6

Baada ya hapo nenda kwenye kipengele cha install, kisha chagua lile file lenye jina la Albe95_Lollirom_V9_DE…FINAL_G.zip ambalo uliliweka kwenye memory card wakati ukiwa kwenye STEP 1. Kisha kubali ku install, na fwatilizia maelekezo kwenye screen ya simu yako.

STEP 7

Baada ya kumaliza ku-install, washa simu yako kisha subiri kama dk 15 maana simu yako itachukua muda kuwaka. Endapo utafanikiwa simu yako itakuwa na muonekano kama kwenye video chini



Kama umependa kazi zetu na unataka tuzidi kusonga mbele basi usiache kutu follow kwenye instagram yetu yenye jina la phonetricktz

No comments:

Post a Comment