Thursday, December 22, 2016

MAUJANJA KWENYE SIMU ZA ANDROID (PART 2)

Simu za android zina maujanja mengi sana. Siku ya leo tutaona ujanja mdogo utakao kuwezesha kuifanya simu yako kuwa ya kipekee na kukupa raha pale unapoitumia.

Leo tutaangalia mambo matatu ambayo watu wengi huwa tunayapita bila kujiuliza yanafanya kazi gani kwenye simu zetu. Window animation scale, Transition animation scale na Animator duration scale. Hayo mambo matatu yanapatikana kwenye kwenye Developer options kama yanavyo onekana kwenye picha chini



Kwenye simu yako utaona Window animation scale, Transition animation scale ni 1x au 1.5x. Ili kuona hivi vitu vina kazi gani basi badilisha Window animation scale kuwa 2x na Transition animation scale kuwa 2x. Kama ujahelewa tazama picha juu kuelewa zaidi. Kisha zima na kuwasha simu yako. Baada ya simu yako kuwaka utaona mabadiliko kwenye speed pale unapofungua app window na unapofunga app window.

Bonyeza part 1 chini kujua maujanja tuliyo jifunza kwenye part 1

Kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram page yetu

No comments:

Post a Comment