Wednesday, December 21, 2016

MUONEKANO MPYA WA GOOGLE KEYBOARD (GBOARD)

Google wanazidi kuiboresha keyboard yao ili kuwa ya kijanja zaidi kushinda keyboard zingine zilizopo kwenye smartphone zetu. Mwanzoni nilikuwa naipenda sana Samsung Keyboard lakini sasa hivi naona pia Google Keyboard ni moja ya keyboard nzuri sanaa kwenye ulimwengu wa smartphone.

Google Keyboard sasa inakuja pamoja na Google Search iki maanisha kwamba unaweza ku search kitu flani kwenye google search bila kutoka kwenye google keyboard. Kwa wale ambao hamjanipata vizuri embu tazama video chini ili kuweza kuelewa nachosema



Kwa wale ambao bado hawaja weka Google Keyboard kwenye simu zao basi unaweza kufanya hivyo kwa kutembelea link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.inputmethod.latin Baada ya kumaliza ku-install kwenye simu yako, utapata muonekano kama picha chini


Bonyeza kipengele kinachosema open kisha utapata monekano kama picha chini


Kisha sogeza (swipe) left kisha utapata muonekano kama picha chini


Bonyeza kipengele kinachosema Select Input Method kisha chagua Gboard. Endapo utafanikiwa utapata muonekano kama picha chini


Bonyeza kipengele kinachosema Set Permissions. Hakikisha una kubali permission za Google Keyboard. Baada ya hapo itapata muonekano kama picha chini


Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka Google Keyboard kwenye simu yako. Kama unataka kuingozea Google Keyboard manjonjo basi nenda kwenye settings za Google Keybaord kisha bonyeza kipengele cha Preferences na utapata muonekano kama picha chini


Kama unataka Keyboard yako iwe na gerefu pamoja na number basi hakikisha kipengele cha number row kipo on kama kwenye picha juu. Kama unataka kubadilisha rangi au muonekano wa keyboard basi nenda kwenye settings kisha nenda kwenye kipengele cha themes.

Kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram page yetu

No comments:

Post a Comment