Friday, November 4, 2016

JINSI YA KUTENGENEZA APP KAMA YA MILLARDAYO (PART 2)

Leo tunaendelea na somo letu ambalo tunajifunza jinsi ya kutengeneza android app kama ya millardayo. Kwa wale wanaotaka kujifunza jinsi ya kutengeneza android app somo hili litakupa ideas ili kukuwezesha wewe kuwa android developer

Hili somo ni part 2 kama kichwa cha habari kinavyosema. Lakini kwenye mtiriko wote wa kujifunza jinsi ya kutengeneza android app hili somo ni part 4

Leo tutajifunza jinsi ya kuweka laucher icon ambayo huwa unabonyeza ndio app ya millardayo inafunguka. Tutatumia picha chini kutengeneza launcher icon yetu.



Application ya android huwa ina mafolder matatu. Folder la kwanza linaitwa Manifest, folder la pili linaitwa Java ambalo huwa linaifadhi mafile yanayo husiana na java code na folder la tatu linaitwa Res au resource ambalo hili folder huwa linaifadhi picha, video, styles, menu, layout ya app yako etc. Hata icon ambayo unabonyeza ili kufungua app husika pia huwa ipo ndani ya folder la res.

Kabla kutengeneza icon ya app ya millardayocopy twende kwenye android studio ili tuone sehemu ipi icon huwa ina kaa. Icon huwa ina kaa kwenye folder linaloitwa mipmap kama linavyo onekana kwenye picha chini



Ukitazama picha juu utagundua kwamba folder la Mipmap ni mtoto wa folder la Res, kwakizungu tunasema ni sub-folder la res. Picha chini inaonyesha ma-folder yote ambayo yapo ndani ya folder la Res na utaona kuna ma-folder 5 ambayo yanaanza na jina la mipmap.



Unaweza kujiuliza haya mafolder matano yenye jina linalo anza na mipmap yana kazi gani kwenye app yetu? Kazi ya haya mafolder ni kuhifadhi launcer icon zenye ukubwa tofauti tofauti kutoka na simu za smartphone zinakuja kwenye ukubwa tofauti.
  • 1:mipmap-mdpi - Hili folder linaifadhi icon kwa ajili ya visimu vyenye display ndogo
  • 2:mipmap-hdpi - Hili folder linaifadhi icon kwa ajili ya simu zenye display kubwa kidogo
  • 3:mipmap-xhdpi- Hili folder linaifadhi icon kwa ajili ya simu zenye display kubwa kidogo zaidi
  • 4:mipmap-xxhdpi - Hili folder linaifadhi icon kwa ajili ya simu zenye display kubwa zaidi kama galaxy S6
  • 5:mipmap-xxxhdpi- Hili folder linaifadhi icon kwa ajili ya simu zenye display kubwaaa kama tablet


Kwa kutumia picha ya millardayo juu ipunguze hadi kufikia ukubwa 192px kwa 192px. Yani upana uwe 192 na urefu uwe 192 kisha save kwenye format ya png na uipe jina la ic_launcher halafu li copy. Kisha nenda kwenye android studio kwenye folder la mipmap halafu right click file lenye jina la ic_launcher.png(xxxhdpi) kisha bonyeza kipengele kinachosena show in explorer kisha paste file ulilo copy hapo.. computer itakuuliza kama unataka ku replace bonyeza ok.

Kwa kutumia picha ya millardayo juu ipunguze hadi kufikia ukubwa 144px kwa 144px. Yani upana uwe 144 na urefu uwe 144 kisha save kwenye format ya png na uipe jina la ic_launcher halafu li copy. Kisha nenda kwenye android studio kwenye folder la mipmap halafu right click file lenye jina la ic_launcher.png(xxhdpi) kisha bonyeza kipengele kinachosena show in explorer kisha paste file ulilo copy hapo.. computer itakuuliza kama unataka ku replace bonyeza ok.

Kwa kutumia picha ya millardayo juu ipunguze hadi kufikia ukubwa 96px kwa 96px. Yani upana uwe 96 na urefu uwe 96 kisha save kwenye format ya png na uipe jina la ic_launcher halafu li copy. Kisha nenda kwenye android studio kwenye folder la mipmap halafu right click file lenye jina la ic_launcher.png(xhdpi) kisha bonyeza kipengele kinachosena show in explorer kisha paste file ulilo copy hapo.. computer itakuuliza kama unataka ku replace bonyeza ok.

Kwa kutumia picha ya millardayo juu ipunguze hadi kufikia ukubwa 72px kwa 72px. Yani upana uwe 72 na urefu uwe 72 kisha save kwenye format ya png na uipe jina la ic_launcher halafu li copy. Kisha nenda kwenye android studio kwenye folder la mipmap halafu right click file lenye jina la ic_launcher.png(hdpi) kisha bonyeza kipengele kinachosena show in explorer kisha paste file ulilo copy hapo.. computer itakuuliza kama unataka ku replace bonyeza ok.

Kwa kutumia picha ya millardayo juu ipunguze hadi kufikia ukubwa 48px kwa 48px. Yani upana uwe 48 na urefu uwe 48 kisha save kwenye format ya png na uipe jina la ic_launcher halafu li copy. Kisha nenda kwenye android studio kwenye folder la mipmap halafu right click file lenye jina la ic_launcher.png(mdpi) kisha bonyeza kipengele kinachosena show in explorer kisha paste file ulilo copy hapo.. computer itakuuliza kama unataka ku replace bonyeza ok.

Kama umeshindwa kutengeneza icon basi tayari nimekuandilia icon zote na unaweza kuzidownload kwa kupitia link chini
https://drive.google.com/file/d/0B2FZbKKFAr42d20xci1faTRKTW8/view?usp=sharing

Kabla ya kujaribisha hii app, kwenye android studio bonyeza alama ya kimshale chenye pembe tatu kwenye kipengele cha Gradle Scripts kisha double click kipengele kinachosema build.gradle(Module:app) na utapata muonekano kama picha chini


NOTE
Kwenye android studio yako badilisha maneno yaliyopo kwenye hicho kipengele ili yafanane na ya kwangu. Sasa kama wewe ni muelewa utaweza kugundua kwamba app yetu itafanya kazi hadi kwenye smartphone zinazotumia android 6, halafu pia utaweza kutambua kwamba version ya app yetu ni 1.0. Tazama picha chini kuelewa zaidi



Sasa umefikia mdaa wa kujaribu app yetu. Kwenye simu yako nenda kwenye settings halafu nenda kwenye kipengele cha Developer Options halafu chini utaona kipengele kinachosema USB debugging kisha kiweke on kama picha inavyo onekana chini.



Chukua USB Cable chomeka kwenye simu halafu chomeka kwenye computer kisha nenda kwenye android studio, bonyeza alama ya pembe tatu yenye rangi ya kijani kama inavyo onekana kwenye picha chini



Endapo utapata ujumbe kana kwenye picha chini basi bonyeza kibox karibu na maneno yanayo sema Always allow from this computer kisha bonyeza ok



Kwenye android studio utaona window mpya inafunga kisha bonyeza jina la simu yako, mfano mimi natumia Samsung SM-N920S, kama inavyo onekana kwenye picha chini


kisha bonyeza ok. Subiri mdaa mchache android studio itaiweka app ya millardayocopy kwenye simu yako. Endapo utafanikiwa basi utapata muonekano kama picha chini



Juu kwenye picha, picha ya kushoto inaonyesha muonekano wa app ya millardcopy na picha ya kulia inaonyesha icon yetu tuliyo itengeneza kwa ajili ya app ya millardcopy

Mpaka hapa tumefikia mwisho, ukitaka kuendelea na hili somo bonyeza Part 5 chini. Kwa wale ambao walikosa masomo yetu yaliyopita basi bonyeza part 1 kujua tulipo anzia.

Kama umependa kazi zetu unaweza kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram page yetu

1 comment:

  1. asante sana mungu awabarikiumenifundisha kitu cha muhimu sana

    ReplyDelete