Saturday, January 7, 2017

JINSI YA KUTENGENEZA APP KAMA YA MILLARDAYO (PART 3)

Mwaka uliopita tulianza kujifunza jinsi ya kutengeneza android application kwa kutumia android studio. Lakini kama unavyojua hili somo ni pana sana na haliwezi kumalizika maana kila kukicha android inazidi kukuwa.

Katika kujifunza kutengeneza android application tulianza na mfano wa kutengeneza app ambayo itafanana na ile ya Millardayo. Kwa wale ambao hawajui tulipo anzia tafadhali bonyeza Part 1 chini ili kufwatilizia mtiririko wa somo hili. Kumbuka hili somo ni part 5

Bila kupoteza mdaa tuendelee na somo letu kwa kufungua Android Studio kisha utaona project yetu ya (Millardcopy). Kama haujaiona nenda kwenye file kisha nenda kipengele kinachosema open recent kisha chagua millardcopy. Kama bado haujaona kitu kama hicho basi rejea part 1 ili ujue tulipoanzia.

Baada ya kufungua Android Studio, Naomba ufungue haya mafile manne (AndroidManifest.xml, MainActivity.java, activity_main.xml, na content.xml). Kama hujui haya mafile yapo wapi basi tazama picha chini ili kuweza kujua hayo mafile yapo wapi. Hakikisha upo kwenye content.xml kama kwenye picha chini


Tukifungua app yetu ya Millardcopy kwenye simu zetu utaona inakwandikia Hello World!. Unaweza ukajiuliza hili neno (Hello World!) limetokea wapi? Hili neno limetokea kwenye content.xml. Ukitazama contect.xml kwenye android studio utagundua hili file lina code zifutwazo

Contect.xml

<relativelayout android:layout_height="match_parent" android:layout_width="match_parent" android:paddingbottom="@dimen/activity_vertical_margin" android:paddingleft="@dimen/activity_horizontal_margin" android:paddingright="@dimen/activity_horizontal_margin" android:paddingtop="@dimen/activity_vertical_margin" app:layout_behavior="@string/appbar_scrolling_view_behavior" tools:context="com.blogspot.phonetricktz.millardcopy.MainActivity" tools:showin="@layout/activity_main" xmlns:android="http://schemas.android.com/apk/res/android" xmlns:app="http://schemas.android.com/apk/res-auto" xmlns:tools="http://schemas.android.com/tools">

<textview
android:layout_height="wrap_content"
android:layout_width="wrap_content"
android:text="Hello World!">
</textview>
</relativelayout>

Sasa kama wewe ni mjanja utagundua kwamba neno Hello World! limetoka kwenye textview element katika attribute ya android:text. Sasa kuelewa zaidi naomba ufute neno Hello World! kisha andika Karibu Phonetrick kama inavyo onekana chini

Contect.xml

<textview
android:layout_height="wrap_content"
android:layout_width="wrap_content"
android:text="Karibu Phonetrick">
</textview>
</relativelayout>

Chukua usb cable yako chomeka kwenye computer kisha chomeka kwenye simu yako kisha test app yetu ya Millardcopy tuone muonekano wake. Kwa wale ambao hawajui jinsi ya ku-test tafadhali soma masomo yetu yaliyopita. Endapo utafanikiwa basi app yetu itakuwa na muonekano kama picha chini



Kabla hatujaendelea embu kwanza tujifunze haya mafile manne yana kazi gani kwenye app yetu (AndroidManifest.xml, MainActivity.java, activity_main.xml, na content.xml).

AndroidManifest.xml

Kila application ambayo unaiona kwenye playstore lazima iwe na AndroidManifest.xml file. Dhumuni kubwa la hili file ni kupeleka taarifa kuhusu application yako kwenye mfumo wa android stystem. Licha ya kupeleka taarifa za msingi, AndroidManifest.xml file inaelezea permissions zote ambazo app yako inataka ili iweze kufanya kazi. Mfano ili hii app yetu ya Millardcopy iweze kufanya kazi ina hitaji ruksa ya kuweza kutumia data. Sitaweza kuelezea mambo yote hapa ukitaka kusoma mwenyewe kuhusu AndroidManifest.xml file basi tembelea link chini
https://developer.android.com/guide/topics/manifest/manifest-intro.html

MainActivity.java

Kama jina linavyosema, mambo yote yanayo husiania na java code basi hapo ndipo yanapopatikana. Code zote za java utakazo andika zinatakiwa ziwepo hapo au kuwa referenced hapo kama utatengeneza java class. Unaweza search google kujifunza zaidi kuhusu MainActivity.java

activity_main.xml na content.xml

Zamani kulikuwa hakuna contect.xml, activity_main.xml ndio ilikuwa inabeba xml zote ambazo zinaonekana kwa mtumiaji wa simu. Mfano kama app yetu inavyo onyesha Hello World au Karibu Phonetrick. Pia Activity_main.xml inaeleza jinsi vitu vitakavyo pangwa ili vionekane vizuri kwenye kioo cha simu yako. Lakini baada ya kuja kwa content.xml basi majukumu yamegawanywa. Content.xml ndio ina xml zote ambazo zinaonekana kwenye kioo chao wakati activity_main.xml ina pangilia jinsi vitu vitakavyo onekana kwenye kioo cha simu yako. Unaweza search google ili kuweza kujifunza zaidi.

Kwenye app yetu kuna baadhi ya vitu tumevikuta ambavyo tunapaswa kujua hivi vitu vimetokea wapi? Mfano kuna Floating Action Button ambayo ina shape ya kama alama ya message. Tazama picha chini ili kuelewa tunaongelea nini



Hicho kialama cha message chenye rangi ya pink ndio kinaitwa Floating Button maana kina helea kwenye screen yako. Sasa swali lina kuja hichi kialama kinapatikana wapi? Hichi kialama kinapatikana kwenye activity_main.xml. Kwenye android studio nenda kwenye file la activity_main.xml chini kabisa utaona maneno ambayo kwenye picha chini yamezungushiwa rangi nyekundu. Hayo maneno ndio yana pelekea sisi kukiona hicho kialama kwenye screen yetu



Kwa leo tuishie hapa. Siku chache zijazo tutaendelea kujifunza namna ya kuifanya hii app ya Millardcopy ifanane kama ile ya mzee wa amplifier aka millardayo. Kwa wale ambao walikosa masomo yetu yaliyopita basi bonyeza part 1 kujua tulipo anzia.

Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram yetu

1 comment:

  1. simu yangu aina ya bird CEO700 kioo chake kimevujia wino nifanyaje?

    ReplyDelete