Tuesday, January 10, 2017

APPS TANO BORA ZA MWAKA 2016

Tukiwa tumefanikiwa kupita mwaka 2016 ni vyema tukaongelea application tano bora ambazo zimefanya vizuri kwenye Android. Kama wengi wetu tunavyojua kwamba mwaka 2016 watumiaji wa android tulipata toleo jipya lenye jina android nougat. Leo tutaona baadhi ya Apps ambazo zimefanya vizuri mwaka 2016.

Gboard


Gboard ni keyboard mpya kabisa kutoka google inc. Baada ya kuwa na Google Keyboard kwa muda mrefu, Google wameiboresha Google Keyboard na kuipa muonekano mzuri na kuipa jina la Gboard. Kwa wale amabao wanataka kuijua vizuri Gboard basi tembelea link chini
http://phonetricktz.blogspot.com/2016/12/muonekano-mpya-wa-google-keyboard-gboard.html

Kwa wale ambao bado hawaja weka Gboard kwenye simu zao basi unaweza kufanya hivyo kwa kutembelea link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.inputmethod.latin

Prisma



Prisma ni moja ya app ambayo imepokelewa vizuri na watumiaji wa android. Hii app inabadilisha muonekano wa picha na kuifanya iwe na muonekano tofauti tofauti. Kwa wale wanaopenda instagram basi hii app siyo ya kukosa. Una weza download prisma kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.neuralprisma&hl=en

Fingerprint Gestures



Hii ni kwa wale wenye simu ambazo zina support fingerprint. Kwa kifupi fingerprint inatumika kama njia ya kulinda mambo yaliyopo kwenye simu yako. Fingerprint Gestures inaongeza matumizi ya fingerprint kwenye simu yako. Kwa kutumia fingerprint gestures unaweza swipe down sehemu ya fingerprint ili kuona notification zako au unaweza ku double tap ili kufungua app flani. Kiukweli fingerprint gestures ni kitu cha kujaribu kama simu yako ina fingerprint scanner. Unaweza download fingerprint gestures bure kutoka kwenye playstore kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.superthomaslab.fingerprintgestures&hl=en

Brave Browser


Kwa wale ambao wanatafuta Browser nzuri zaidi ya Google Chrome basi jibu ni Brave Browser. Brave Browser ni bure kabisa kwenye playstore ikija na uwezo wa kuzuia matangazo pale unapo peruzi. Pia inakupa ulinzi dhidi ya virus ambazo zinaweza kusababisha simu yako isifanye kazi katika kiwango kinacho stahili. Unaweza download brave browser bure kutoka kwenye playstore kwa kutumia link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.brave.browser&hl=en

Snapseed



Snapseed ni app ambayo imezinduliwa na Google kwa ajili ya ku-edit picha. Kwa wale wapenzi wa ku-edit picha basi hutakiwi kukosa Snapseed kwenye simu yako. Licha ya kuwa na mambo mengi mazuri, Wabongo tunapenda mteremko kwahiyo Google wameamua kuitoa bure Snapseed bila hata kulipia cent tano. Kama unataka snapseed basi tembelea link chini
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.niksoftware.snapseed&hl=en

Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram yetu

No comments:

Post a Comment