Tuesday, January 17, 2017

KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA KUHUSU SCREEN TO BODY RATIO

Screen to body ratio ni kiasi cha nafasi ambacho kioo cha simu yako kinachukua kati ya nafasi yote ya muonekano wa mbele wa simu yako. Simu nyingi zitakazo toka mwaka 2017 zitakuwa zinashindana kwenye swala la screen to body ratio.

Zipo baadhi za company ambazo tayari zimesha tengeneza simu ambazo kioo kinachukua nafasi zaidi ya asilimia 90%. Unaweza kujiuliza hii ni simu gani ambayo kioo chake kinakaribia kufunika muonekano wote wa mbele? Xiaomi Mi Mix ni simu ambayo imewaacha watu wengi midomo wazi kwa kuweza kufanya kioo kichukue karibia nafasi yote ya muonekano wa mbele. Tazama picha chini ujionee mwenyewe jinsi Xiaomi Mi Mix ilivyo.



Kwa wale ambao wanataka kuona simu ikichambuliwa kwa undani zaidi basi usiache kutazama video chini


Samsung nao wanadai kwamba samsung galaxy S8 inakuja na screen to body ratio kwa asilimia 90%.. Mhhhh... Kuakikisha hili swala Samsung wametoa video za matangazo kuhusu kioo cha AMOLED na katika hii video watu wengi wanadhani simu ambayo inaonekana kwenye hizo video inaweza kuwa ni Samsung Galaxy S8... Unaweza kutazama hizo video mbili chini kisha unaweza kutoa mawazo yako kama unadhani hiyo simu kwenye video ni Samsung Galaxy S8.





Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram yetu

No comments:

Post a Comment