Monday, January 23, 2017

KWA NINI GALAXY NOTE 7 ILIKUWA INAWAKA MOTO?

Samsung ilifanikiwa kuuza Galaxy Note 7 million 3 na kati ya hizo asilimia 96% zilirudishwa kutoka na hatari ya kuwaka moto. Samsung wametoa video ikieleza sababu iliyopelekea hadi Galaxy note 7 kuwaka moto

Wachunguzi 700 kutoka Samsung walijaribu kupima Galaxy Note 7 ili kugundua ni kitu kinacho sababisha hii simu kushika moto? Wachunguzi hao waliweza kugundua sababu mbili zilizopelekea Galaxy Note 7 kuwaka moto. Sababu ya kwanza ni makosa yaliyo fanyika katika kuweka nyaya za negativie ambazo zilijipinda kutoka na electro deflection, Sababu ya pili ni cheche ya ajabu inayotokea kwenye battery ambayo inapelekea simu kupiga shoti na kuanza kuwaka moto. Matatizo yote hayo yana toka kwenye battery.

Kutokana na hayo matatizo hapo juu, Samsung wamechukua hatua kali kuakikisha mambo kama hayo yasitokee tena. Moja ya hatua walizochukua ni kufanya test nane mbali mbali za kupima battery ili kuakikisha battery ina usalama kwa watumiaji. Na pia wamechunguza vifaa vingine vilivyomo ndani ya simu kwa kutumia X-rays ili kuakikisha vipo imara.

Unaweza check video ambayo Samsung wateoa kueleza sababu zilizopelekea Note 7 kuwaka moto na hatua walizochukua ili kutokomeza tatizo


Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram yetu

No comments:

Post a Comment