Wednesday, January 25, 2017

KWA NINI CYANOGENMOD NA CYANOGEN OS ZIMEKUFA?

Kwa wale ambao wamezoea kuweka custom rom kwenye simu zao, neno CyanogenMod sio kitu kipya. Kwa kifupi CyanogenMod ni android open source project ambayo ilitolewa kwa matumizi mmbadala ya stock android. Mfano mgonjwa anaye sumbuliwa na maumivu ya kichwa anaweza kutumia panadol au hedex..

CyanogenMod iliendelea kufanya vizuri na kuweza kutapakaa kwenye simu nyingi. Baada ya mafanikio makubwa ya CyanogenMod yalipelekea kuzinduliwa kwa mfumo mpya uliopewa jina la Cyanogen Os.

Kwa kuwa CyanogenMod ilikuwa bure basi Cyanogen Os ilikuja ili iweze kuingiza hela kwa kuuzwa na kutumiwa kwenye smartphone badala ya stock android. Moja ya kampuni iliyoanza kutumia Cyanogen Os kwenye simu zao ni OnePlus. OnePlus one ndio simu iliyoanza kutumia mfumo wa Cyanogen Os. Tazama picha chini ya OnePlus One



Cyanogen Os iliendelea kufanya vizuri, na mmoja wa waanzilishi wa CyanogenOs Steve Kondik aliibuka na kusema kwamba anataka kuifuta stock android ya Google na kuifanya Cyanogen Os kuteka ulemwengu mzima. Mhhh... yani hapa ni sawa na kusema mtoto mchanga ampige baba yake hadi kufa halafu mtoto awe baba.... hahahaaaaaa.....

"Microsoft decided to partner instead of buy or invest: Microsoft was taking a wait-and-see attitude with Cyanogen. She said that "Cyanogen is doing something fairly basic" and that "at this time, it feels like it makes more sense to partner to see how its journey is going," adding that "partnerships are sometimes about exploring." But she says, other options are not completely off the table. "We’ll stay close to them and continue to look of more ways to partner," she said."

Baada ya Steve Kondik kutamka maneno hayo, haikuchukua hata miaka miwili ndipo taarifa zilipo anza kuenea kwamba Steve Kondik anaondoka na kuicha Cyanogen Os. Baadae kidogo taarifa zikatoka kwamba Cyanogen Os haita endelea tena na itafungwa na simu ambazo zinatumia mfumo wa Cyanogen Os hawata pata tena updates. Mpaka sasa hivi ninavyo andika hapa, Cyanogen Os pamoja na baba yake CyanogenMod zimefungwa tayari na simu zinazotumia hizi rom mbili hazitapata tena updates.

Story haijaishia hapo, baada ya Steve Kondik kuondoka, inasemekana amekwenda kuanzisha mfuo mwingine mpya wa android ambao utatumika kwa matumizi mmbadala ya stock android. Yaani kwa kifupi story ni kama imeanza mwanzo. Tayari mfumo huo umepewa jina la Lineage Os. na umeshaanza kutumika kwenye simu mbali mbali kama Nexus 6P.

Sababu moja kubwa iliyopelekea Cyanogen Os na baba yake CyanogenMod kufa ni uongozi mbaya.. kwa kizungu wanasema poor management. Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram yetu

No comments:

Post a Comment