Sunday, January 29, 2017

MAMBO MAPYA YALIYOMO KWENYE EMUI 5.0

EMUI kirefu chake ni Emotional User Interface. Kwa wale wanaotumia simu za Huawei basi tayari watakuwa wanafahau kuhusu emui. Kwa kifupi Emui ni mfumo ambao Huawei wanauweka juu android ili kuifanya huawei kuwa na muonekano tofauti pale unapo ilinganisha na simu nyingine kama Samsung au LG.

Kila kampuni huwa inaweka muonekano wake wa kipekee kwenye simu zao ili kuzifanya ziwe na muonekano wa kipekee. Mfano Samsung wanaweka Touchwiz, HTC wanaweka HTC Sense, Tecno wanaweka Hios na Huawei wanaweka EMUI.

Katika EMUI 5.0 ambayo inakuja na android 7 (Nougat), Huawei wamezidi kuiboresha Emui kwa kuipa rangi nzuri zinazovutia kama white and blue. Pia wameongeza app drawer launcher ambayo haikuwepo kwenye EMUI zilizopita.



Huawei hawajaishia hapo, Moja ya kitu mizuri kabisa kilicho ongezwa ni App twin ambayo inakusaidia kuendesha app moja mara mbili. Mfano wengi tunajua huwezi tumia Facebook mbili kwenye simu moja au huwezi tumia whatsapp mbili kwenye simu moja. Sasa usikariri kwenye emui 5 mambo kama hayo yanawezekana.

Screen Gestures ni jambo lingine ambalo Huawei anaendelea kuliwekea mkazo kwenye EMUI 5.0. Kwa wale ambao hawajui nini maana ya Screen Gestures ni kwamba ni zile shortcuts ambazo unaweza kuzifanya kwa kupitia kioo cha simu yako. Mfano kwenye emui 5.0 unaweza kuchora alama S na simu yako itafanya screenshot au unaweza kukunja kidole chako na kuchora mstari katikati ya kioo chako na simu yako itagawanyika mara mbili na utaweza kufanya multi-tasking.

Mambo ni mengi ambayo yameongezwa kwenye EMUI 5.0 na kama unataka kuyajua yote basi usiache kutazama video chini



Kama umependezwa na kazi zetu basi usiache kutufwata kwenye instagram page yetu ya phonetricktz

No comments:

Post a Comment