Wednesday, February 1, 2017

SIMU KALI TANO AMBAZO UNAWEZA KUNUNUA SASA HIVI

Mdaa mwingine huwa ni vigumu sana kuchagua simu maana zipo simu nyingi sanaa sokoni lakini ni shida sanaa kujua ipi ni bora kushinda nyingine. Leo nitataja simu tano tu ambazo zina ubora kila kona.

HUAWEI MATE 9



Kiukweli Huawei wanajitahidi sana kutoa simu nzuri na zenye bei nafuu sanaa. Huawei Mate 9 ni moja ya simu nzuri sana na inakuja na android 7 (nougat) kutoka kwenye box. Hii simu ina urefu wa 156.9mm, upana wa 78.9mm na uzito wa 190g.

Kioo chenye ukubwa wa 5.9" FHD Display. Kwa wale ambao hawajui maana ya FHD ni FULL HIGH DEFINITION . 4GB RAM.. jamani... 64GB ukubwa wa ndani au kwa kizungu internal storage. Pia kwa wale wanaopenda kuweka memory card basi utaweza kuweka memory yenye ukubwa hadi kufikia 256GB. Camera ya nyuma ina 20 Megapixels na ya mbele ina 8MP halafu unaweza kurecord video za 4K.... Mambo ya ku record video kwenye Full High Definition yashapitwa na wakati, sasa hivi 4K ndio mpango mzima.

Simu ina uwezo wa kutumia line mbili.. SIM card 1 itatumia 4G LTE na SIM card 2 utaweza kutumia 3G.. mhh... wengi tunajua simu za line mbili moja inakuwa na 4G na nyingine inakuwa na 2G.. Kwenye Mate 9 mambo kidogo ni tofauti. Nisiongee sana ukitaka kuijua hii simu vizuri basi tembelea link chini
http://consumer.huawei.com/en/mobile-phones/tech-specs/mate9-en.htm

LG V20



LG V20 naye ni mnyama mwingine anayekuja na android 7 (nougat) kutoka kwenye box. Kioo chenye ukubwa wa 5.7 inch Quad HD (High Definition). Simu inakuja na USB Type-C™ pamoja na Qualcomm® Quick Charge™ 3.0*. Battery ina ukubwa wa 3,200 mAh na unaweza kuitoa pia Simu ina 64GB internal Storage RAM 4GB na inaweza kutumia memory card hadi yenye ukubwa wa 2TB..Dah dah.....

Camera ya nyuma ina ukubwa wa 16MP na ile ya mbele ina ukubwa wa 5MP. Unaweza pia kuchua slow motion video. Simu ina uwezo wa kutumia line moja. 4G LTE kama kawaida. Kiukweli LG V20 sio simu ya mchezo unaweza kujua sifa zake nyingine kwa kutembelea link chini
http://www.lg.com/us/mobile-phones/v20/specs

SAMSUNG GALAXY S7 & S7 EDGE

Kitu cha kwanza kabisa ambacho Samsung Galaxy S7 kinayo ni uwezo wa kutoingia maji. Hii ina maanisha utaweza kutumia simu yako hata sehemu yenye mvua au hata ukiwa sehemu za starehe kama beach au kwenye swimming pool.

Samsung Galaxy S7 inakuja moja kwa moja kutoka kwenye box na android (6.0.2)marshmallow. Unaweza ku-update na kutumia android 7 (Nougat). Samsung Galaxy S7 ina kioo chenye ukubwa wa 5.1-inch screen na 2,560x1,440-pixel resolution pamoja na processor ya Qualcomm Snapdragon 820 pamoja na 4GB ya RAM. Samsung Galaxy S7 pamoja na Samsung Galaxy S7 Edge zote zina camera ya nyuma yenye 12 megapixel. Kujua zaidi kuhusu hii simu unaweza tembelea link chini
https://phonetricktz.blogspot.com/2016/02/samsung-galaxy-s7-kipi-unachotakiwa.html

ONEPLUS 3T

Never Settle ni slogan ya OnePlus, mimi binafsi napenda sana hiyo Slogan. Turudi kwenye OnePlus 3T, Hii ni simu ambayo ina Ram kubwa hadi kufikia 6GB na memory ya ndani hadi 128GB. Kwa kifupi ukiwa na hii simu hauitaji tena Memory card. Camera ya nyuma na ya mbele ina ukubwa wa 16MP . Pia OnePlus 3T inakuwezesha kuchukua video za 4K.

Bei ya hii simu ni $439 sawasawa na 1,010,000 Tanzanian Shillings. Uzito wa hii simu ni 158g urefu wa 152.7mm na upana wa 74.7mm. Kioo cha hii simu ni Corning® Gorilla® Glass 4, 1080p Full HD. Ukitaka kuijua hii simu kwa undani basi tembelea link chini
https://oneplus.net/3t/specs

Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram yetu

No comments:

Post a Comment