Monday, February 20, 2017

WHATSAPP YATIMIZA MIAKA 8 TANGU KUANZISHWA. INA KUJA KIVINGINE NA KI SOCIAL ZAIDI.

Penda usipende, Whatsapp ni moja ya mtandao ambao unatumiwa na watu wengi kushinda mitandao yote ya kijamii. Whatsapp wanadai kwamba kwa siku moja message hadi kufikia bilioni 50, video zisizo pungua milioni 760 pamoja na Gif zinazo fikia millioni 80.

Miaka 8 iliyopita (February 2009), whatsapp ilikuwa ipo kwenye matengenezo na sasa whatsapp imekuwa moja ya kitu muhimu sana katika maisha yetu. February 24 2017, whatsapp itakuwa inasherekea kufikisha miaka nane na inakuja na zawadi kubwa kwa watumiaje wake. Whatsapp sasa wanaboresha kipengele cha status na kitakuwa kina jitegemea.

Watu tutakuwa na uwezo wa kuweka status ya maneno, video, picha, Gif na marafiki zako wataweza ku comment pia utakuwa una uwezo wa kuzia baadhi ya watu wasione status yako. Hii ina maanisha kwamba status itakuwa kama page flani ambayo utaweza ona marafiki zao wana post nini na post zitakaa kwa mdaa wa masaa 24... hahahaaaaaaaaaaaaaaaaa

Ebwana nisiongee sanaa, unachotakiwa kufanya usisahau ku-update whatsapp yako February 24 2017. Tazama picha chini kuona kionjo ambacho whatsapp wamekiweka kwenye blog yao kuhusiana na mpango wao wa kuboresha status.



Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram yetu

No comments:

Post a Comment