Monday, February 13, 2017

KIPI UNACHOTAKIWA KUJUA KUHUSU INSTANT APP

Mwaka jana kwenye kongamano la Google I/O 2016, Google walitambulisha mfumo mpya wa apps unao julikana kama Instant Apps. Huu mfumo bado haujaanza kutumika kwenye simu za android lakin siku chache zijazo tutaanza kuona mfumo huu ukianza kutumika.

Instant apps hizi ni app ambazo utaweza kuzitumia bila ya kuzi install kwenye simu yako. Idea ni kwamba uki search kitu kwenye google, mfano amazon, kama amazon wana instant app utaweza kutumia hiyo app bila kuweka amazon app kutoka kwenye playstore na utwaweza kufanya manunuzi, kuangalia bidhaa na ukimaliza hiyo app ya amazon itajifunga na haitakuwepo kwenye simu yako. Tazama video chini kuelewa zaidi jinsi instant app inavyo fanya kazi



Kitu kingine kizuri zaidi, Google wanadai kwanza instant app zitafanya kazi hadi kwenye android za nyuma kama android 4.1 Jelly Bean. Mpaka hapo tumefikia mwisho, Kama umependa kazi zetu usiache kutufwata kwenye instagram yetu ya phonetricktz au bonyeza picha chini kutembelea instagram yetu

No comments:

Post a Comment