Friday, October 13, 2017

JINSI YA KUANDIKA MANENO YENYE BOLD AU ITALIC KWENYE WHATSAPP

Wale wapenzi wa kuchat kwenye Whatsapp tayari washakutana na message ambazo zina maneno ya bold, italic,monospace na Strikethrough. Kwenye picha juu kuna baazi ya maneno yanaonekana yana bold

Leo ntaonyesha ujanja kidogo ambao watu wengi bado hatuujui..Cha kwanza ili uweze kufanya yote kirahisi ningekushauri kwanza download Gboard Keyboard kutoka kwenye playstore. Kama huna hiyo Gboard Keyboard tembelea link chini ili uweze kuipakua
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.google.android.inputmethod.latin

Sasa kama tayari umesha install Gboard Keyboard na ndio umeifanya iwe ni keyboard inayotumika. Kama bado hujui jinsi ya kufanya hivyo basi tembelea link chini
https://phonetricktz.blogspot.com/2016/12/muonekano-mpya-wa-google-keyboard-gboard.html?m=1

Sasa mfano unataka kuandika maneno yenye Bold. Fungua Whatsapp yako kisha andika ujumbe wako halafu kabla haujautuma kwa mtu select yale maneno ambayo unataka yawe na bold mfano kwenye picha chini utaona mimi nimeselect maneno yanasomema hivi See, I have told you beforehand. Matthew 24:21‭-‬22‭, ‬25 NKJV



Sasa kama unataka hayo maneno yawe na bold, baada ya kuselect maneno yako bonyeza ile alama ambayo ina mistari mitatu kama inavyo onekana kwenye picha chini



Baada ya kubonyeza hiyo alama utaona kuna vipengele vifwatavyo.. Bold
Italic
Monospace
Strikethrough
Kama inavyo onekana kwenye picha chini.

Mfano ukichagua bold maneno yataonekana kama ifwatavyo



Mfano umechagua Italic< basi maneno yataonekana kama ifwatavyo



Mfano umechagua Strikethrough basi utapata muonekano kama picha chini

Unaweza jaribu Monospace kuona itakuwaje.. Mpaka hapo tumefikia mwisho wa somo letu.. Kama unapenda kazi zetu usiache kutu follow kwenye instagram yetu ya phonetricktz

1 comment:

  1. As reported by Stanford Medical, It is indeed the one and ONLY reason women in this country get to live 10 years more and weigh an average of 42 lbs less than we do.

    (And realistically, it really has NOTHING to do with genetics or some secret diet and really, EVERYTHING related to "how" they are eating.)

    BTW, What I said is "HOW", not "WHAT"...

    Click this link to discover if this brief quiz can help you decipher your real weight loss potential

    ReplyDelete