Sunday, February 22, 2015
TRAILER FUPI YA SAMSUNG GALAXY S6.. #NEXT GALAXY
Samsung Galaxy S6 inatarajiwa kutoka tarehe 1 mwezi March pamoja na HTC M9. Miaka michache iliyopita Samsung wamejikuta wakipoteza soko la smartphone na kupelekea mauzo ya simu zao kupungua.
Wengi wamekuwa waki lalamika simu za Samsung kuwa nzito kutokana na kuweka application nyingi kama Samsung Gear, Group Play, Snote, S Planner, S Reminder etc ambazo watu wengi hawazitumii na wanaona hazina maana. Kibaya zaidi hizo zote application huwezi kuzi toa (uninstall) kwenye simu yako.
Kitu kingine ambacho Simu za Samsung zina lalamikiwa sana ni System UI (USER INTERFACE). Samsung hutumia Touchwiz kwenye simu zao lakini developers wengi wamekuwa wakisema kwamba touchwiz ipo slow na inatumia Ram nyingi ili kufanya kazi ukilinganisha na Sense UI ambayo inatumika sana kwenye simu za HTC
Swala lingine ambalo Samsung wamekuwa waki lalamikiwa sana ni kuhusiana na material yanayotumika kutengeneza muonekano wa nje kwenye simu za Samsung. Samsung wanapenda sana kutumia material ya plastic ambayo wengi wanasema inafanya samsung ionekane kama simu ya bei rahisi ukilinganisha na iphone au HTC.
Samsung wamesikia vilio vya watu na wamesema kwamba Samsung Galaxy S6 itakuwa tofauti sana na marekebisho mengi yamefanyika kwe System UI (touchwiz) na pia application kama Samsung Gear, Group Play, Snote, S Planner, S Reminder utaweza kuzitoa kabisa kwenye Samsung Galaxy S6 kama utapenda kuzitumia.
Inasemekana kwamba Samsung Galaxy S6 itatumia material ya alluminium kwenye muonekano wake wa nje. Hii itaifanya Samsung Galaxy S6 kuwa imara na kuonekana ni simu ya gharama kama ilivyo iphone.
TRAILER YA SAMSUNG GALAXY S6.. #NEXT GALAXY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment