Wednesday, April 15, 2015

JINSI YA KUBADILISHA MUONEKANO WA HUAWEI Y300


Kama wewe ni mtumiaji wa Huawei Y300 leo utaweza kujua jinsi ya kubadili muonekano wa simu yako kwa kutumia themes.

Themes zimeanza kutumika kwa kasi kama njia ya kubadilisha muonekano wa simu yako. Kwa wale ambao wanatumia rom za cyanogenmod wao watakuwa wameshaanza kufaidika na themes.

Kwa sasa tayari tushatoa maelekezo jinsi ya kuweka cyanogenmod kwenye Huawei Y300 na kwenye Samsung Galaxy GTI9300.
Leo nitatoa maelekezo jinsi ya kubadili muonekano wa Huawei Y300 kwa kutumia themes.










JINSI YA KUBADILISHA MUONEKANO WA HUAWEI Y300 KWA KUTUMIA THEMES

STEP 0
Hakikisha tayari umeweka rom ya cyanogemmod kwenye Huawei Y300. Kama bado ujaweka rom ya ya cyanogemmod temebelea link chini kujua zaidi
http://phonetricktz.blogspot.com/2015/04/jinsi-ya-kuweka-cyanogenmod-kwenye.html

STEP 1
Download green theme kutoka kwenye playstore kwa kutumia link chini kisha install kwenye simu sako.
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.ronapps.theme.greenuifree

STEP 2
Kwenye simu yako bonyeza menu button ambayo ipo chini kulia na utaona muonekano kama picha chini


STEP 3
Bonyeza sehemu iliyoandikwa themes na utaona muonekano kama picha chini



STEP 4
Bonyeza kipengele kilichoandikwa theme packs na utapata muonekano kama picha chini



STEP 5
Bonyeza kipengele kinachoitwa Green UI kisha tick kipengele kinachoitwa style kisha bonyeza apply.


Mpako hapo utakuwa umefanikiwa kubadili muonekano wa simu yako ya Huawei Y300 kwa kutumia themes.
Kama ungependa kuwekewa cyanogenmod kwenye simu yako unaweza wasiliana nasi kupitia namba +255716203029 na utatozwa gharama ya Tsh 25,000.

Unaweza ku-like our facebook page or you can follow us on instagram #phonetricktz.

No comments:

Post a Comment