Monday, April 20, 2015

JINSI YA KUTATUA TATIZO LA "YOUR BOOT/RECOVERY IMAGE MAY HAVE AN INCORRECT SIGNATURE." KWENYE HUAWEI Y300


Kwa wale wenye Huawei Y300 ambao wamekutana na haya maneno  "YOUR BOOT/RECOVERY IMAGE MAY HAVE AN INCORRECT SIGNATURE." pale wanapowasha simu sasa tatizo hilo linaweza kutatulika.

Kwanza nieleze sababu ambayo inaweza kupelekea mtu kukumbana na tatizo kama hilo. Sababu ya kwanza ni kujaribu kuweka custom recovery kabla huja unlock bootloader. Sababu nyingine ni kujaribu ku unlock simu za huawei ambazo zimekuwa locked to one network. Kufanya hivi inaweza ikasababisha simu yako ikafa moja kwa moja na usiweze kuitumia tena.



Hili tatizo nimewai kukutana nalo na pia watu wengi wamekuwa wakiomba maelekezo jinsi ya kutatua hili tatizo kwenye simu ya Huawei Y300.

VIGEZO NA MASHARTI VYA KUZINGATIA

  1. MIMI SITAHUSIKA ENDAPO UTAARIBU SIMU YAKO
  2. HAKIKISHA UNA UWELEWA KIDOGO WA COMPUTER
  3. GENERAL COMMON SENSE IS REQUIRED
  4. WINDOW PC IS REQUIRED NOT AN OPTION

JINSI YA KUTATUA TATIZO LA "YOUR BOOT/RECOVERY IMAGE MAY HAVE AN INCORRECT SIGNATURE." KWENYE HUAWEI Y300

STEP 0
Download HuaweiY300v1.1.exe kwa kutumia link chini kisha install kwenye computer yako
https://mega.co.nz/#%21zI5XgA4S%21YwI3ixgn-v4-yPNfQek6XCDW4NZkexD2fNdoVw77S68

STEP 1
Baada ya ku-install program nenda kwenye local disk kisha hakikisha folder lenye jina la HuaweiY300 AIO lipo ndani ya program files na sio program files(x86). Kama lipo ndani ya
program files(x86) hakikisha unalipeleka (move) kwenye program files. Endapo hutafanya hivyo basi program yako haitafanya kazi



STEP 2
Baada ya kuliamisha folder lenye jina la HuaweiY300 AIO kwenda program files, lifungue hilo folder kisha ndani utakuta mafolder matatu. Fungua folder linaloitwa tools kisha utaona mafolder mawili. Fungua folder linaloitwa unlocktools kisha utaona mifile yafutayo


STEP 3
Double click program inayoitwa HuaweiY300 ambayo ipo ndani ya unlocktools folder na kisha click button inayoitwa Install driver ambayo ipo kushoto juu kabisa


STEP 4
Download Huawei USB Driver kwa kutumia link chini kisha extract hilo file kisha utapata folder linaloitwa huawei usb driver. Fungua hilo folder kisha utapata muonekano kama picha chini
https://www.dc-unlocker.com/download/Huawei_usb_driver_2.0.6.601.zip



STEP 5
Kama computer yako ni 64 bit operating system unatakiwa ku double click DriverSetup64 kama computer yako sio 64 bit operating system basi double click DriverSetup kisha subiri mpaka installation imalizike.

STEP 6
Bonyeza kipengele kinachosema Bootloader Code kisha subiri kidogo kisha  itafunguka program inayoitwa DC unlocker ambayo inamuonekano kama picha chini



STEP 7
Kwenye simu yako ya Huawei Y300 toa battery subiri kama sekunde 30 kisha rudishia battery halafu shikilia kwa pamoja button ya kuongeza sauti na kupunguza pamoja na button ya kuwashia kwa mpaka screen yako itakapokuwa ya pink. Kwa kutumia usb cable chomeka simu yako kwenye computer.

STEP 8
Kwenye program yako ya DC unlocker, kipengele kinachosema "select manufacturer" unaweka huawei phones na kipengele kimachofwatia unakiacha kama kilivyo kisha bonyeza duara lenye alama ya kutafuta kisha subiri na utapata muonekano kama picha chini. Kisha copy sehemu bootloader code yako ambayo ina tarakimu(digits) 16.

NOTE
Hakikisha computer yako ipo connected na internet



STEP 9
Zima simu yako ya huawei y300 kisha toa battery suburi kama 5sec kisha rudisha battery halafu bonyeza na kushikilia kitufe cha kupunguza sauti (vol down) kisha bonyeza cha kuwashia (power button). Vishike vitufe hivyo viwili kwa muda wa sekunde 10 kisha chomeka simu yako kwenye computer kwa kutumia usb cable

STEP 10
Kwenya program yako ya Huawei Y300 kama inavyo onekana kwenye STEP 3  bonyeza button inayosema 1 Unlock bootloader. Kisha andika ile unlock code ambayo ina tarakimu 16 uliyoipata kwenye STEP 8. na bonyeza inter kwenye computer yako. Kisha bonyeza enter tena. Utaona message inayosema bootloader imekuwa unlocked successfully na simu yako itajizima na kujiwasha yenyewe. 

Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kutatua tatizo la  YOUR BOOT/RECOVERY IMAGE MAY HAVE AN INCORRECT SIGNATURE. 

Kama umeshindwa na unataka msaada kutoka kwetu utatakiwa kulipa Tsh 30,000. Piga simu na +255753877552.


No comments:

Post a Comment