Leo nitatoa malekezo jinsi ya kuweka cyanogenmod kwenye Huawei Y300. Moja ya faida utakayopata baada ya kuweka cyanogenmod kwenye Huawei Y300 ni kubadili muonekano wa simu yako kwa kutumia themes na kuifanya simu yako kuwa na uwezo mkubwa
JINSI YA KUWEKA CYANOGENMOD KWENYE HUAWEI Y300
STEP 0
Hakikisha simu yako ipo rooted na ume unlock bootloader na pia umeweka custom recovery. Kama bado tembelea link chini kwa msaada zaidi
STEP 1
Download Nebula Cyanogenmod 11 rom kwa kutumia link chini kisha weka hilo file kwenye memory card.
STEP 2
Download Google Apps (GAPPS) kwa kutumia link chini kisha weka hilo file kwenye memory card
STEP 3
Download CWM Recovery kwa kutumia link chini kisha weka hilo file kwenye memory card
STEP 4
Zima simu yako. Washa simu yako kwenye recovery mode.
NOTE
Kuwasha simu kwenye recovery mode unatakiwa ushikilie cha kuwashia na cha kuongeza sauti kwa wakati moja na usiviachie mpaka utakapoona logo ya huawei imepotea kwenye screen ya simu yako.
STEP 5
Bonyeza kipengele cha Install kisha juu kabisa bonyeza sehemu iliyoandikwa internal sdcard na chagua kipengele kinachosema Micro sdcard
STEP 6
Flash lile file ambalo ume download kwenye STEP 3 (recovery-clockwork-6.0.4.5-u8833-R3.zip)
kisha toa battery halafu rudishia na washa simu yako kwenye recovery mode tena (STEP 4) na utaona
muonekano kama picha chini
STEP 7
Kwa kutumia button ya kupunguza sauti nenda hadi kwenye kipengele kinachosema backup and restore kisha
bonyeza button ya kuwashia simu. Kisha nenda tena hadi kwenye kipengele kinachosema
backup to /sdcard/sdcard1 kisha bonyeza tena button ya kuwashia.
NOTE
backup huwa inachukua kama dakika tatu au mbili kumalizika. Umuhimu wa backup ni kuweza kuirudisha simu yako kama ilivyokuwa endapo itakupa matatizo baada ya kuweka cyanogenmod.
STEP 8
Baada ya kumaliza ku backup, rudi nyuma kisha nenda kwenye kipengele kinachosema
wipe data / factory reset kisha bonyeza button ya kuwashia.
STEP 9
Nenda kwenye kipengele cha advanced kisha bonyeza cha kuwashia halafu nenda kwenye kipengele
kinachosema wipe dalvik cache
STEP 10
Nenda kwenye kipengele kinachosema install zip kisha bonyeza cha kuwashia kisha nenda kwenye
kipengele kinachosema choose zip from /storage/sdcard1
STEP 11
Nenda hadi kwenye lile file ambalo uli download kwenye STEP 1 ambalo linaloitwa Nebula_V1.0.4.zip
kisha bonyeza cha kuwashia. Subiri mpaka simu yako imalize ku flash.
STEP 12
Nenda hadi kwenye lile file ambalo uli download kwenye STEP 1 ambalo linaloitwa pa_gaaps-modular-really-micro..
kisha bonyeza cha kuwashia. Subiri mpaka simu yako imalize ku flash.
STEP 13
Reboot simu yako. Kisha baada ya simu yako kuwaka nenda kwenye about phone na utaona
unatumia cyanogenmod
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa kuweka cyanogenmod kwenye Huawei Y300. Endapo umekwama na ungependa
kusaidiwa unaweza wasiliana nasi kupitia namba +255765659669 na gharama zitatozwa kiasi cha Tsh 25000 tu.
No comments:
Post a Comment