Friday, June 5, 2015

JINSI YA KUWEKA FLOATING TOOLBOX KWENYE SIMU ZA ANDROID


Floating Toolbox ni app ambayo inakusaidia kufungua app unazopenda kutumia kwa haraka zaidi. Kama jina linavyosema "Floating Toolbox App" huwa inaelea kwenye screen ya simu yako na unaweza kuitumia muda wowote.

Toolbox ilianzia kwenye simu za Samsung na baadae ilianza kusambaa kwenye simu nyingine amabazo zinatumia mfumo wa android. Leo tutaangalia jinsi ya kuweka na kuitumia floating toolbox kwenye simu yako.



JINSI YA KUWEKA FLOATING TOOLBOX KWENYE SIMU ZA ANDROID

STEP 0
Download Floating Toolbox kwa kutumia link chini au nenda kwenye playstore kisha tafuta app inayoitwa Floating Toolbox kisha install kwenye simu yako.
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.kimcy92.toolbox

STEP 1
Fungua Floating Toolbox app kisha ruhusu  kipengele kinachosema enable toolbox kama picha inavyo onyesha  chini


STEP 2
Juu kabisa utaona kipengele kinachosema "Select Apps" kisha chagua apps ambazo unataka ziwe kwenye toolbox



STEP 3
Baada ya kukamilisha steps zote kwa umakini utaona kiduara ambacho ndani yake kuna vidoti vitatu. Bonyeza hicho kiduara halafu utaona app zako zote ambazo umechagua zikielea kwenye screen yako na utaweza kuzitumia wakati wowote.


Kwa mfano,
Picha chini zinaonyesha mimi nikiwa na uwezo wa kufungua app yoyote ninayotaka nikiwa kwenye instagram, facebook, youtube na kwenye browser




Floating Toolbox pia inakuwezesha kubadilisha rangi na kuchagua rangi ambayo wewe binafsi unapenda. Ukitaka Kubadili rangi ya floating toolbox nenda kwenye settings

Mpaka hapo tumefikia mwisho wa maelekezo ya kuweka floating toolbox kwenye simu yako

Kwa wale wanaopenda blog yetu na wanataka tuendele zaidi basi usiache kutufwata kwenye instagram kupitia phonetricktz 

No comments:

Post a Comment