Friday, November 21, 2014

JINSI YA KUBALISHA RANGI YA STATUSBAR PAMOJA NA VIALAMA KWENYE SIMU ZA ANDROID



Android inasifika kwa mambo mengi sana mojawapo ikiwa ni uwezo  wa mtumiaji kubadilisha muonekano wa android na kuweka muonekano ambao yeye binafsi anaupenda



Leo tutajifunza jinsi ya rangi ya vialama vilivyo kwenye statusbar. Vialama hivyo ni kama alama ya battery, network, aina ya network pamoja na saa. Pia tutabadilisha rangi ya statusbar. Statusbar ni ile sehemu ya juu kabisa kwenye kioo chako cha simu. Sehemu iyo ndio inatumika kuonyesha notification za apps pamoja na kuonyesha alama ya network, battery etc.

Picha chini inaonyesha jinsi rangi ya statusbar pamoja na vialama vya battery, network, saa vilivyo badilika rangi




Kama umependa muonekano huo hapo juu na ungependa uweke kwenye simu yako soma maelekezo chini

JINSI YA KUBALISHA RANGI YA STATUS BAR PAMOJA NA VIALAMA VILIVYO KWENYE STATUSBAR

STEP 1
Hakikisha umeweka Gravity Box kwenye simu yako. Kama bado tembelea link chini
http://phonetricktz.blogspot.com/2014/11/jinsi-ya-kuweka-gravity-box-kwenye-simu.html

STEP 2
Fungua Gravity Box kwenye simu yako na utapata muonekano kama huo hapo chini

STEP 3
Bonyeza kipengele cha statusbar tweaks kisha utaona muonekano kama huo hapo chini


STEP 4
Bonyeza sehemu iliyoandikwa statusbar colors kisha  enable icon colors utaona  alama ya on kama picha hapo chini
SSTEP 5
Nenda kwenye kipengele cha statusbar background color na chagua rangi unayoipenda kama picha inavyoonyesha chini

STEP 6
Nenda kwenye kipengele cha statusbar icon color kisha  fanya kama ulivyofanya kwenye step 5.

Mpaka hapo tumefikia mwisho natumaini utakuwa umeelewa. Kama umepata tatizo toa maoni yako chini na utajibiwa. Usiache ku like Facebook page yetu.


No comments:

Post a Comment